NYUMBA 23 ZATEKETEZWA KWA MOTO MPANDA

Mussa Mwangoka, SumbawangaMGOGORO baina ya wafugaji na wakulima umeibuka tena baada ya wakazi wa Kijiji cha Majalila, Kata ya Mpanda ndogo ,wilayani Mpanda kuchoma moto nyumba 23 za wafugaji kwa madai mifugo yao imeharibu mazao katika mashamba ya wakulima.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 asubuhi katika kijiji hicho, baada ya wakazi wapatao 500 kuendesha msako kijijini hapo wenye lengo la kuwachomea nyumba wafugaji wote wa ng’ombe wanoishi kijijini hapo
Katika tukio hilo la uchomaji wa nyumba za bati na nyasi kwenye baadhi ya nyumba zilitoka nyoka hali ambayo iliwafanya wakazi hao kuziua na kisha kugawana vipande vipande kwa imani za kishirikina.
Habari zaidi kutoka Mpanda zilieleza kuwa wananchi hao waliamua kujichukulia sheria mkononi za kuchoma nyumba hizo kwa kile walichokieleza kuwa uongozi wa Serikali ya Kijiji umeshindwa kuwachukulia hatua wafugaji hao kila wanapopelekewa uharibifu wa mazao ya mahindi na tumbaku.
Aidha Polisi walipopata taarifa na kufika kwenye eneo hilo wakiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Joseph Myovela akiwa na baadhi ya wajumbe wa ulinzi na usalama wa wilaya hiyo kwa lengo la kwenda kutuliza vurugu hizo, walijikuta kwenye wakati mgumu baada msafara wao kuzuiwa na wananchi hao waliokuwa na hasira kali huku wakiwa na silaha za jadi.
Hata hivyo mkuu wa polisi aliweza kuwatuliza wakazi hao baada ya kuwapa maelezo ya muda mrefu na ndipo walipopunguza jazba na kisha wakakubali waweke mkutano baina ya wakazi wa kijiji hicho na viongozi wa wilaya.
Kwenye mkutano huo, Siadi Maninge ambaye ni mmoja wa wakulima alisema hali hiyo imetokana na matatizo yanayosababishwa na Viongozi wa Serikali ya kijiji ambao wamekuwa wakiwapokea wafugaji wenye makundi makubwa ya mifugo na kuwakaribisha kijijini hapo bila kujali eneo lililopo halitoshelezi kwa kilimo na ufugaji mkubwa.
Naye Diwani wa Kata ya Mpanda ndogo, Khamadi Mapengo alisema kama uongozi wa serikali ya kijiji utafuata sheria na taratibu, migogoro ya namna hiyo haitatokea, hivyo wana kila sababu ya kufuata taratibu katika utendaji wao wa kazi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.