OBAMA ATETEA UAMUZI WA KUTUMA JESHI LIBYA

Rais Barack Obama hahitaji idhini ya bunge la congress kuwatuma wanajeshi wa Marekani kuhusika katika operesheni za Nato nchini Libya.
White House inasema wanajeshi wa Marekani wanahusika katika majukumu madogo sana nchini LibyaKulingana na maelezo ya ikulu ya White House, Rais Obama ana uhuru kutuma wanajeshi hao kama kiongozi wa taifa.
Lakini kulingana na sheria iliotungwa wakati wa vita vya Vietnam, rais wa Marekani lazima apate idhini ya bunge la congress kutuma wanajeshi kuhudumu katika nchi ya kigeni ikiwa muda huo utachukua zaidi siku sitini.
Wabunge nchini Marekani wanasema Rais Obama amekiuka sheria hio kwa kuwa muda wa siku sitini ulikwisha mwezi May 20.
Lakini White House imewasilisha taarifa katika bunge hilo, ikielezea kuwa jukumu la wanajeshi wa Marekani ni la kusaidia tu kikosi cha Nato.
White House imesema majukumu ya jeshi la Marekani nchini Libya sasa hivi hayajafikia kiwango ambacho kimewekwa kwenye sheria hiyo ya mwaka wa 1973 ambapo rais atalazimika kuomba idhini ya congress.
Wanjeshi wa Marekani wanasaidia kuongeza ndege za Nato mafuta na katika shughuli za kijasusi nchini Libya, kulingana na maelezo ya White House.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa wanajeshi wa Marekani hawapo kwenye makabiliano na jeshi la Libya, kwa hivyo hawako vitani.
Kulingana na katiba ya Marekani, bunge la congress ndio lenye uwezo wa kutangaza vita.
Ifikiapo jumapili wiki hii, Marekani itakuwa imehusika kwenye harakati hizo za Nato nchini Libya kwa jumla ya siku tisini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA