OUT YAMWAGIWA NA tbl MILIONI 40 ZA MAJI

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Profesa Tolly Mbwette akimuonesha Meneja Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kushoto) eneo la Makao Makuu ya OUT lililotengwa kwa ajili ya viwanja mbalimbali vya michezo, katika Kijiji cha Bungo, Wilayani Kibaha, Pwani. TBL ilialikwa na uongozi wa OUT kuishukuru kwa kuwapatia msaada wa mabomba ya maji yenye thamani ya sh. milioni 40.Kulia ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu.


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Profesa Tolly Mbwette (kulia) akimuonesha Meneja Miradi Maalum wa TBL, Emma Oriyo, Jengo la kuhifadhia vifaa na nyaraka mbalimbali za chuo hicho lililopo Makao Makuu hayo mapya.




Meneja Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kushoto), akielezea mbele ya vyombo vya habari chuoni hapo leo, sababu zilizowafanya watoe msaada wa mabomba ya maji katika chuo hicho.




Renatus Mashimba ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Fabcast iliyo karibu na chuo hicho ambayo pia itafaidika na msaada huo, akisoma risala ya shukurani kwa TBL katika hafla hiyo.







Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Profesa Tolly Mbwette (kushoto) akisoma risala ya shukurani kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa kukipatia chuo hicho msaada wa mabomba ya mfumo wa maji yenye thamani ya sh. milioni 40 katika hafla iliyofanyika leo Makao Makuu mapya ya OUT, yaliyopo katika Kijiji cha Bungo, Kibaha, mkoani Pwani. Kulia ni Meneja Miradi Maalum wa TBL, Emma Oriyo.








Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI