RAIS BASHIR KUFUNGA MABOMBA YA MAFUTA

Rais Bashir wa Sudan

Rais Bashir kufunga mabomba ya mafutaRais Omar al-Bashir wa Sudan ametishia kufunga mabomba yanayosafirisha mafuta kutoka Kusini mwa Sudan ikiwa mpango muafaka kuhusu suala la mafuta hutoafikiwa kabla Sudan Kusini kuanza kujitawala mwezi Julai.


Amesema Sudan Kusini inaweza kuendelea kutoa nusu ya pato lake la mafuta kwa Sudan Kaskazini ama ilipie kutumia miundombinu ya Kaskazini katika utaratibu wa kusafirisha mafuta.
Ninaipa Sudan Kusini mapendekezo haya..chaguo ni lake, Sudan Kaskazini iendelea kupata fungu lake ama ipokee malipo kwa kila pipa linalotumwa kutoka Sudan Kusini kwenda bandarini "Rais Omar al BashirBw. Bashir amesema ikiwa hakuna litakalozingatiwa kati ya hayo mawili basi atafunga mabomba yote ya mafuta.
Theluthi tatu ya mafuta ya Sudan yako Sudan Kusini lakini mabomba mengi, viwanda vya kusafishia mafuta na bandari kuu vyote viko Sudan Kaskazini.
Sudan Kusini ilipiga kura ya maoni mwezi January kutaka kujitawala.
Mambo matatu
Rais Bashir alitoa vitisho hivi katika hotuba yake aliyoitoa mjini Port Sudan kuliko bandari kuu inayotumika kusafirisha mafuta.Hotuba yake hiyo ilionekana katika televisheni ya taifa.
Mazungumzo bado yanaendelea kati ya Kaskazini na Kusini mwa Sudan kuhusu mafuta na masuala mengine nyeti kabla ya Sudan Kusini kujitawala, ikiwa ni pamoja na suala la uraia na lile la eneo linalozozaniwa la Abyei.
Mwezi jana, jeshi la Sudan Kaskazini lilikamata eneo la Abyei lakini kumekuwa na makubaliano yalioafikiwa Jumatatu ambayo yanatoa fursa ya kuondolewa wanajeshi hao kutoka eneo hilo na kupelekwa wanajeshi wa Ethiopia katika eneo hilo kudumisha amani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.