RPC KILIMANJARO AFARIKI DUNIA

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro,Kamishna msaidizi
mwandamizi wajeshi la polisi (SACP),Lucas Ng’hoboko (pichani) amefariki dunia gafla
baada yakuanguka.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kaimu kamanda wa polisi mkoanihumo,Yusuph Ilembo alisema kuwa kifo hicho kilitokea Juni 17 Majira
yasaa 3 asubuhi katika zahanati ya polisi mjini hapa.
Alisema taarifa za awali zinaeleza kwamba kamanda huyo alifikishwakatika zahanati ya polisi kwa ajili ya kuangalia afya yake lakinikabla suala hilo halijatekelezwa alianguka gafla na kupoteza maisha.
Ilembo alisema Ng’hoboko ambaye alikuwa katika likizo ya kustaafutangu Juni mosi mwaka huu,hakuwa anasumbuliwa na maradhi yoyote
hadikifo chake kilipotokea.
“Ni kweli kamanda Ng’hoboko amefariki dunia leo asubuhi…hii
imetushtuasana,hakuna anayefahamu sababu za kifo chake,tunasubiri taarifa zakitaalamu kutoka kwa madaktari”alisema.
Kaimu kamanda alisema kwa sasa mwili wake umehifadhiwa katikahospitali ya rufaa ya KCMC kwa ajili ya uchunguzi na baadaye taratibuza mazishi kufanyika kwa maelekezo ya familia yake.
Marehemu Ng’hoboko alihamia mkoani Kilimanjaro mwaka 2006,baada
yamkuu wa jeshi la polisi nchini,Said Mwema kufanya mabadiliko yakumhamisha aliyekuwa kamanda Venance Tossi ambaye naye alimpokeakamanda Mohamed Chico.
Marehemu Ng’hoboko alianza rasmi likizo ya kustaafu Juni mosi mwakahuu na kwamba kamanda wa polisi mkoani Pwani,Absolom Mwakyomaanatarajiwa kuhamia rasmi mkoani humo Julai mwaka huu.
Baadhi ya askari ambao hawakutaka kutajwa Majina
yao,wamezungumziamaisha ya marehemu,Ng’hoboko kwamba alikuwa kiongozi aliyejali
maslahiya askari wake na kuwasikiliza wote bila kujali vyeo wala umriikilinganishwa na viongozi wengine.
Walisema baadhi ya maafisa wa jeshi huvunja mahusiano na kutowajaliaskari waliopo chini yao ikiwa ni mara baada ya kupata nafasi za juukatika jeshi hilo jambo ambalo halikuwa likifanywa na marehemuNg’hoboko.
Kwa upande wao wakazi wa mji wa Moshi,Abdalah Ali na John Mushiwalisema wakati wa uongozi wa marehemu Ng’hoboko alijitahidi
kudhibitimatukio ya ujambazi ikilinganishwa na miaka mingine iliyopita.
“Siyo vizuri kufurahi jinsi polisi walivyokuwa wakifanya mauaji lakinikwa kiasi Fulani mauji yale yalipunguza matukio ya ujambazi mkoaniKilimanjaro…hii ilikuwa kazi nzuri ya kamanda Ng’hoboko,Mungu
amlazepema peponi”alisema Mushi.
kwa habari zaidi juu ya kifo hicho endelea kutembelea mtandao huu ama
sikiliza radio Uhuru Fm kwa habari moto moto
Imewekwa na Francis Godwin ni Iringa na matukio 0 Maoni Links to
this post

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.