RWANDA YACHAPWA NA URUGUAY

Rwanda U 17

Rwanda yachapwa na Uruguay Goli katika dakika za majeruhi kutoka Uruguay, lilizima matumaini ya Rwanda kupata pointi yake ya kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 17.


Licha ya kupoteza mchezo huo, Rwanda bado kimahesabu ina nafasi ya kusonga mbele na kuingia katika timu 16, iwapo itashinda mchezo wake wa mwisho katika kundi c watakapocheza na Canada, juni 25.
Goli hilo pekee kwenye mchezo uliochezwa nchini Mexico lilipatikana katika dakika tano za nyongeza, baada ya kipa wa Uruguay kupiga mkwaju wa adhabu uliomkuta Leonardo Paris aliyefunga kwa kichwa.
Rwanda ilianza mchezo huo vizuri, na ilimiliki mpira mapema, na hata kupata nafasi za karibu kufunga magoli, kutokana na mipira miwili ya adhabu iliyopigwa na nahodha Emery Bayisenge.
Mkwaju wa kwanza uligonga mwamba, la wa pili ukipita juu kidogo ya mwamba.
Mtiririko wa timu ya Rwanda maarufu kama Dondola watoto, uliharibika baada ya meneja Richard Tardy kulazimika kufanya mabadiliko, kutokana na jeraha la goti la beki Faustin Usengimana.
Uruguay ilinufaika na mabadiliko hayo, na kuaza kufanya mashambulizi.
Rwanda ilifanikiwa kupiga mikwaju miwili katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda yoyote.
Uruguay ilimiliki kipindi cha pili.
Ushindi huu unamaanisha Uruguay wanasonga mbele katika timu 16, na watapambana na England Juni 25. England walitoka sare ya 2-2 na Canada katika mchezo mwingine wa kundi c.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU