SERIKALI KUIBEBA U -23

SERIKALI imesema itaisaidia kwa hali na mali timu ya taifa ya vijana ya U-23 kwa kuwatafutia wadhamini na kuwatafutia kocha mpya ambaye atakuwa akiinoa timu hiyo ambayo kwa sasa inanolewa na Jamhuri Kihwelo 'Julio'.
Timu hiyo kwa sasa iko kambini ikijiandaa na mchezo wa marudiano na Nigeria 'Flying Eagles' kuwania kucheza Michezo ya Olimpiki itakayofanyika London mwakani.
Kauli hiyo ya serikali ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara wakati hakijibu swali la nyongeza la Mbunge wa (Nungwi), Yusuph Haji Khamis aliyetaka kufahamu mpango wa serikali kuisaidia timu hiyo.
Mukangara ambaye alitumia nafasi hiyo kuwapongeza U-23 kwa kushinda mchezo wao dhidi ya Nigeria na kuongeza kuwa serikali ipo pamoja nao katika maandalizi yao ya kuelekea katika mashindano ya Olimpiki yanayofanyika mwakani Uingereza.
Hata hivyo, Naibu Waziri huyo alisema kwa sasa hali ya soka nchini iko juu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo makocha wa kigeni kutoka nje ya nchi ambao waliiwezesha timu ya taifa kupanda viwango vya FIFA kutoka 167 mwaka 1995 hadi kufikia 86 mwaka 2008.
Wakati huo huo, Jessca Nangawe anaripoti kuwa wachezaji wa U-23, Mbwana Samata, Jabir Aziz na golikipa Shaaban Kado watajiunga na wenzao leo katika mazoezi yanayoendelea kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Nigeria.
Wachezaji hao ambao walikua wakilitumikia taifa wakati Taifa Stars ilipocheza na Afrika ya kati wamerejea na kujumuika na wenzao ambapo leo watajumuika katika amzoezi yatakayoendelea katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Naye kocha wa timu ya U-23 ya Nigeria, Austin Eguavoen amesema Vijana Stars ya Tanzania hawana nafasi ya kusonga mbele ya mashindano hayo kwa mgongo wao.
Eguavoen aliliambia gazeti la Vanguard la Nigeria: "Kwa kuwa ni mechi ya mechi mbili, tumepoteza nafasi nyingi za kufunga Dar es Salaam, hapa lazima tufunge...lazima tuwatoe Tanzania."
Hata hivyo, kocha huyo wa zamani wa Super Eagles, alikiri kuwa Tanzania ina wachezaji wazuri lakini akasisitiza pamoja na uzuri wao, wakija Nigeria hawatoki.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.