TP MAZEMBE KUWASILISHA RUFAA FIFA

KIKOSI CHA TP Mazembe kilichochuana na Simba, jijini Dar

Wachezaji wa TP Mazembe wakishangilia moja ya mabao
Mazembe kuwasilisha rufaa yake kwa FIFAMabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani Afrika, TP Mazembe, kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imesema itawasilisha rufaa yake kwa shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA, badala ya mahakama ya upataishi ya michezo CAS.


Shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF, iliipiga marufuku TP Mazembe kutetea taji lake baada ya Klabu ya Simba ya Tanzania, kulalamikia uamuzi wa klabu hiyo wa kumshirikisha Janvier Besala Bokungu kama mchezaji wake.
Awali klabu ya TP Mazembe, ilisema itawasilisha rufaa yake kwa mahama ya upatanishi ya micheszo CAS.
Lakini baada ya muda wa mwisho kuwadia, bila ya Mazembe kuwasilisha rufaa yake, Klabu hiyo imesema itawasilisha malalamishi yake kwa FIFA.
Klabu hiyo kutoka DRC, iliishinda Simba kwa jumla ya mabao 6-3 katika raundi ya pili ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Afrika, lakini Simba ikahoji uhalali wa Bokungu kuichezea Mazembe.
TP Mazembe, imeteuwa mawakili kutoka Ubelgiji Luc Mission na Gregory Ernes kuwasilisha rufaa yao kwa FIFA.
Wachezaji wa TP Mazembe kabla ya mechi yao dhidi ya Simba ya TanzaniaBokungu, mwenye umri wa miaka 22 mzaliwa wa Congo, alihamia klabu ya Esperance ya Tunisia kutoka Mazembe mwaka wa 2007 na kujiunga tena na klabu Mazembe mapema mwaka huu.
Ripoti zinasema Bokungu, alikiuka mkataba wake na Esperance ambao ungemalizika mwezi june mwaka huu, lakini mawakili wa Mazembe wanasema uhamisho wa mchezaji huyo ni halali.
Mazembe imeshinda kombe la klabu bingwa barani Afrika kwa miaka miwili iliyopita na pia ilifuzu kwa fainali za kombe la klabu bingwa ulimwenguni, ambapo ilishindwa 3-0 na klabu ya Inter Millan, kutoka Italia.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.