TRENI SUDANI KUSINI YASHAMBULIWA

Treni katika mji Aweil, Sudan
Treni iliyobeba wananchi wa Sudan Kusini kurudi nyumbani kutoka Kaskazini imeshambuliwa na kundi la Kiarabu kutoka kaskazini na kusababisha kifo cha mtu mmoja, Umoja wa Mataifa umesema.
Msemaji wa Umoja huo alisema treni hiyo ilishambuliwa na kundi la Misseriya wenye silaha katika jimbo la Kordofan Kusini Jumapili ingawa kiongozi wa kundi la Misseriya alikanusha.
Takribani watu 70,000 wameyakimbia mapigano ya hivi karibuni katika jimbo la Kordofan linalopakana na Sudan Kusini.
Wasiwasi umekuwa ukiongezeka huku Kusini ikielekea kupata uhuru wake mwezi ujao.
Watu wengine 100,000 wamelazimika kuyakimbia makazi yao baada ya mapigano katika eneo lenye mzozo la Abyei, karibu na Kordofan Kusini.
Tangu kumalizika kwa vita vya Kusini na Kaskazini miaka 21 iliyopita, Wasudani Kusini wapatao milioni mbili wamerejea nyumbani na wengine zaidi wanaendelea kurudi kabla ya kutangazwa kwa uhuru
wao Julai 9.
"Treni iliyokuwa ikiwasafirisha Wasudani Kusini waliokuwa njiani kutoka Kosti kwenda Wau ilishambuliwa na wapiganaji wa Misseriya," alisema msemaji wa UN Hua Jiang.
Hata hivyo, kiongozi wa Misseriya Mohamed Omer al-Ansary alisema shambulio hilo limefanywa na waasi katika eneo jirani la Darfur, ambako mgogoro tofauti ulitokea mwaka 2003.
Majeshi ya Kaskazini yamekuwa yakilaumiwa kwa kulipua baadhi ya sehemu katika Kordofan Kusini yanayokaliwa na kabila la Wanuba, ambao wamekuwa wakiunga mkono Kusini wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mapigano yalizuka baada ya makundi yanayounga mkono Kusini kuamriwa kunyanga’anywa silaha baada ya Ahmed Haroun kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa karibuni wa ugavana.
Bwana Haroun anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu Darfur.
Mwishoni mwa wiki Bwana Haroun alisema hali sasa ni shwari na watu wameanza kurejea kwenye makazi yao.
Hata hivyo Shirika la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International limeshutumu mamlaka kulazimisha watu kurejea warejee kwenye makazi yao ilhali bado kuna mapigano yanaendelea.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.