U 23 v NIGERIA OLIMPIKI

U 23 v NIGERIA OLIMPIKITimu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ambayo Jumamosi (Juni 18 mwaka huu) itacheza ugenini na Nigeria katika mechi ya marudiano ya mchujo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani London, Uingereza itaagwa kesho. U 23 itaagwa saa 7 mchana kambini F&J Hotel iliyoko Mikocheni, Dar es Salaam. Mechi dhidi ya Nigeria itachezwa Uwanja wa Samuel Obgemudia ulioko Benin City, ambapo ni kilometa 320 kutoka Jiji la Lagos. Waamuzi wa mechi hiyo ambao wote wanatoka Senegal ni Ousmane Fall (mwamuzi wa kati), Maguette Ndiaye, Cheikh Toure na mwamuzi wa akiba Daouda Gueye. Kamishna ni Emmanuel Zombre kutoka Burkina Faso. Boniface WamburaOfisa Habari

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU