UTAJIRI WA WAHUBIRI NIGERIA WAKITHIRI

Wahubiri wa Nigeria wamefanikiwa katika miradi yao na kuwa na utajiri unaolinganishwa na matajiri wanaofanya biashara ya mafuta.
Kwa mujibu wa muandishi wa blogu moja huko Nigeria aliyefanya utafiti wa wahubiri hawa wa neno la Mngu ameiambia BBC kuwa wana Biashara kabambe utadhani wana visima vya mafuta.

Mfonobong Nsehe, mwandishi wa blogu ya jarida la kibiashara la Forbes anasema kuwa ma- pastor wanamiliki biashara kubwa kuanzia hoteli kubwa hadi biashara za chakula, mfano wa vyakula vya haraka kama vile 'nyama na kuku'' sawa na Kentucky' ambazo ni vivutio kwa familia na vijana.
Mwandishi huyu anasema kuwa"Uhubiri ni biashara kubwa. Faida yake ni sawa na biashara ya mafuta ya petroli.
kituo cha mafuta
Alitowa mfano wa utajiri wa Wahubiri watano ambao wana takriban dola milioni 200m.
Kanisa za wahubiri wa aina hii zimeimarika nchini Nigeria katika miaka ya hivi karibuni, ambapo maelfu kwa maelfu wameshiriki na kujiunga nazo.
Bw.Nsehe anasema Mhubiri anayeongoza kwa utajiri, Bishop David Oyedepo wa Kanisa lijulikanalo kama Living Faith World Outreach Ministry, alikadiriwa kuwa na utajiri wa takriban dola milioni150.
Bishop Oyedepo anamiliki kampuni ya kuchapisha, Chuo kikuu, shule moja ya msingi ya kifahari, ndege zake nne za binafsi za kifahari na nyumba kadhaa mjini London na Marekani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.