VIONGOZI WAJADILI SOKO LA PAMOJA AFRIKA



Viongozi wajadili soko la pamoja Afrika

Viongozi wa Afrika wanakutana mjini Johannesburg kutayarisha mpango wa kuwa na biashara huru kutoka kusini hadi kaskazini mwa bara hilo yaani Cape hadi Cairo.

Nchi 26 kutoka Jumuiya tatu za Afrika zinahudhuria kikao hicho ili kuondoa vikwazo vya biashara na kuifanya Afrika kuwa kama soko moja, linalofanana na Umoja wa Ulaya.

Hakuna shaka kuwa Afrika ina mali, na nchi nyingi sasa zinaibuka vema kutoka msuko-suko wa kiuchumi wa dunia.

Ikiwa nchi za Afrika zitafungua mipaka yake na kuwa soko huru kutoka Cape Town hadi Cairo, basi itazidisha biashara baina yao.

Hivi sasa nchi nyingi za Afrika zinafanya biashara na mataifa yaliyozitawala zamani au Uchina, badala ya kuwa na ushirikiano wa kibiashara na jirani zao.

Wazo la kufungua mipaka lilitolewa kwenye mkutano uliofanywa nchini Uganda mwaka wa 2008 lakini mazungumzo yalisita kwa sababu ya msukosuko wa uchumi wa dunia.

Kazi ya mkutano wa sasa mjini Johannesburg ni kutatuwa matatizo yaliyokuwako na kupanga mwongozo wa kufwata, ili kutekeleza mpango.

Jumuiya za Afrika Mashariki, COMESA na SADC zinahudhuria mkutano huo ila ni Jumuiya ya Afrika Magharibi tu, ECOWAS ambayo haijatuma wajumbe.

Majimbo hayo matatu yana watu milioni 600 na asili-mia-60 ya pato la Afrika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.