WAKULIMA WAPIGWA MARUKU KUUZA VYAKULA NJE YA NCHI

KATIKA kukabiliana na hali mbaya ya chakula, Mkoa wa Manyara umezuia uuzaji mazao nje ya nchi na kupiga marufuku matumizi ya nafaka kutengenezea pombe.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Manyara (Ras), Claudio Bitegeko, hatua hiyo inatokana na hali ya mavuno ya mazao kwa baadhi ya maeneo ya mkoa kutoridhisha.Bitegeko alisema mazao mengi mkoani humo, yamedumaa hivyo kusababisha matarajio ya mavuno kwa wakulima kutoweka, jambo linaloashiria kuwapo kwa njaa siku za usoni.

“Miongoni mwa maeneo yanayotarajiwa kuathirika kwa kiasi kikubwa na hali hiyo, ni halmashauri za wilaya ya Simanjiro, Kiteto na maeneo ya Yaeda Chini na Masieda, Wilaya ya Mbulu, Mamire, Endakiso na Nkaiti wilayani Babati,” alisema Bitegeko.

Hata hivyo, Bitegeko alisema tayari mkoa umechukua hatua mbalimbali za kusaidia wananchi kukabiliana na hali hiyo, ikiwamo kuomba chakula cha msaada kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Maafa na tayari wamepata tani 1,601.

Katibu Tawala huyo alisema halmashauri za wilaya zilizopata msaada huo, ni mji wa Babati tani 1,000 na Wilaya ya Simanjiro tani 601.Alisema hatua nyingine waliyochukua ni kushauri wananchi kupitia viongozi wa mkoa, wilaya na halmashauri, kuhifadhi mazao ya kutosha baada ya mavuno, kwani kila mtu kwenye kaya moja anatakiwa kuweka akiba ya magunia matatu ya mahindi kwa ajili ya matumizi ya mwaka.

“Wafugaji wenye idadi kubwa ya mifugo wanatakiwa wauze baadhi ya mifugo yao, ili wanunue chakula na wakulima wanatakiwa kuuza mazao yao ya biashara na kutumia fedha zitakazopatikana kununua mazao ya chakula,” alisema.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA