WALIOACHWA WAIDAI SIMBA

SIKU moja baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuweka wazi wachezaji saba wa Simba ambao wanatakiwa kupelekwa katika timu nyingine kwa mkopo, wachezaji wawili wa timu hiyo wameugomea uongozi wao na kudai kuwa hawako tayari kwenda timu yoyote.
Simba kupitia Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, lilitangaza kuwaacha wachezaji saba, huku ikitangaza kuwatoa kwa mkopo Meshack Abel, David Naftali, Mohamed Kijuso, Ally Ahmed 'Shiboli', Haruna Shamte na Juma Jabu.
Mbali na wachezaji hao, wachezaji watatu waliuzwa katika klabu za TP Mazembe ya DRC na Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wachezaji hao walidai kuwa wanadai fedha nyingi za usajili, mishahara na posho na kwamba hawaendi popote huku baadhi yao wakidai kuwa hawajashuka kiwango kama ilivyodaiwa na uongozi wa Simba.
Beki wa Simba, Meshack Abel alisema pamoja na kusoma kwenye magazeti, taarifa za kutolewa kwake kwa mkopo, lakini uongozi haujamwambia lolote kuhusu hilo.
Meshack ambaye mwaka juzi Simba walimpeleke African Lyon kwa mkopo na baadaye kumrudisha katika dirisha dogo baada ya beki wao tegemeo George Owino kuumia na kushindwa kucheza karibu nusu msimu mzima.
Alisema yeye hayuko tayari kwenda kwenye timu yoyote ile kucheza kama mchezaji wa mkopo anachoitaji ni kupewa haki yake ili aweze kuwa huru.
''Mimi sina taarifa yoyote na hata kama watanipa taarifa hiyo sitakuwa tayari kucheza timu nyingine tena ninachotaka ni Simba wanipe haki zangu zote kwani nawadai fedha nyingi,'' alisema Meshack.
Naye mshambuliaji wa timu hiyo ambaye alisajiliwa katika dirisha dogo Ali Ahmed Shibori alisema kuwa kwa upande wake hataki hata kusikia kupelekwa kwa mkopo katika timu nyingine kwani ni bora harudi zake Pemba akacheze kwenye timu za kwao.
Wakati Shibori akisema hayo, David Naftali alisema "Sijapata barua yoyote ya Simba ikinitaarifu kuuzwa kwa mkopo, nitakuwa tayari kwenda iwapo tu watanitafutia timu yenye upinzani katika ligi sipo kwa ajili ya Simba," alisema Naftali
"Mpira kwangu ni ajira na nipo kimaslahi, naamini kuna timu nzuri zaidi kuliko hiyo Simba na Yanga ambazo zinawezeshwa ndio maana zina ushindani, lakini kuna timu ambazo haziwezeshwi na zina ushindani mkubwa tena zina uwezo kuliko hizo Simba na Yanga, umri wangu unaniruhusu kucheza zaidi.''
Alisema tayari ameanza mazungumzo na timu mbalimbali na anachoangalia hivi sasa ni dau la kila timu kabla hajaamua kumwaga wino.
Naye Mohamed Kijuso alisema: "Nataka nikutane kwanza na viongozi wa Simba niongee nao kabla sijatoa maamuzi yangu, mpaka sasa sijapata barua yoyote ya viongozi ikinijulisha suala hilo," alisema Kijuso.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI