WAZIRI MMOJA ATAJWA KUCHOCHEA MGOGORO WA UVCCM ARUSHA

Katibu wa CCM, Mkoa wa Arusha, Marry Chatanda
WAZIRI mmoja ametajwa kuhusika kuchochea mgogoro baina ya Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM) na Katibu wa chama hicho mkoani Arusha, Mary Chatanda.Kigogo huyo ametajwa kufadhili kundi mojawapo la vijana kwa lengo la kuwachafua viongozi wenzake ndani ya chama hicho na serikali.
Vyanzo vya habari vya uhakika vimelieleza gazeti hili kuwa, tuhuma dhidi ya waziri huyo (jina limehifadhiwa kwa sasa) ziliibuliwa miongoni mwa vijana wanane walihojiwa juzi mbele ya Tume ya Maadili na Usalama ya CCM, iliyofika Arusha hivi karibuni kwa lengo la kuchunguza na kupata ufafanuzi kuhusu mvutano huo.
Taarifa zinadai kuwa, waziri huyo anayeshikilia wizara nyeti alitajwa kuwa ni miongoni mwa watu waliochangia mgogoro huo, kwa kufadhili kada maarufu wa UVCCM mkoani hapa (jina limehifadhiwa) Sh60 milioni, lengo likiwa ni kutafuta vijana wataoendesha mapambano ya kuwapinga na kuwachafua viongozi wenzake ndani ya chama na serikali.
Kwa mujibu taarifa hiyo iliyotolewa kwaa tume hiyo, waliamua kusema ukweli juu ya tuhuma hizo zinazomkabili waziri huyo kwa lengo la kumaliza mvutano ulioshika kasi.
“Sisi tuliamua kuieleza tume kuwa huyu waziri ametoa kiasi cha fedha kwa kumpatia kada mwenzetu wa UVCCM, kwa lengo la kuondoa unafiki hatuwezi kuwa wanafiki kama tunataka kumaliza haya mambo ndugu yangu," walisema kwa nyakati tofauti.
Hata hivyo, vyanzo hivyo vya habari vilikwenda mbali zaidi na kuliambia gazeti hili ya kuwa, tume hiyo juzi ilimhoji Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM mkoani hapa, Mrisho Gambo, kuhusiana na mvutano uliopo baina ya jumuiya na Chatanda.
Taarifa hizo zinadai kuwa Gambo alihojiwa na tume hiyo juzi kabla ya kikao cha kamati ya siasa mkoa hakijakaa na kujadili mapendekezo yaliyowasilishwa na tume hiyo.
Pia, tumea hiyo inadaiwa kuwahoji vijana wawili wa UVCCM mkoani hapa, waliotambulika kwa majina ya Ally Babu, ambaye ni katibu hamasa wa vijana Kata Levolosi na Masoud ambaye ni Katibu wa Vijana wa CCM Kata ya Lemara.
Katika hatua nyingine, taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya vijana ambao walihojiwa na tume hiyo hivi karibuni zimedai kuwa, kuna mpango wa kuwaengua ndani ya chama hicho baadhi ya wanachama wa chama hicho akiwamo Mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa, James Ole Milya.Wengine wanaotajwa kutakiwa kuenguliwa ni Ally Majeshi, Ally Banaga na Nyiti wa Arumeru.
Millya alikiri kupata taarifa hizo huku akisema kuwa mpango huo hauwezi kufanikiwa kwa sababu, anawakilisha hisia na hoja za vijana wa CCM.




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI