Ofisa Uhusiano wa Pensheni ya Watumishi wa Serikali (PSPF), Fatma Elhady (kushoto), akitoa maelezo kwa watumishi wa umma, jinsi ya kukamilisha ujazaji fomu za pensheni katika maadhimisho hayo yanayofikia kilele kesho kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakiangalia mashine ya kukoboa nafaka iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga la Jeshi la Wananchi Tanzania (JWZT). Mashine hiyo inayouzwa sh. 1,200,000 inaoneshwa kwenye maadhimisho hayo.
Ofisa Kumbukumbu wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ismail Said (kushoto), akitoa maelezo kwa wananchi, jinsi wanavyotambua vitu mbalimbali kwa kutumia vinasaba (DNA), katika maadhimisho hayo.
Mkaguzi Mwandamizi wa Vyakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Moses Mbambe akionesha mvinyo ambao ni sehemu ya vyakula na dawa feki zinazooneshwa kwenye banda la TFDA, katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa na Afrika yanyofikia kilele leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)

Comments