4x4

JK KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA AFRIKA (AU)

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na baadhi ya marais wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika AU wakimpongeza Rais mstaafu wa Brazil Lula Da Silva kwa hotuba yake aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Wakuu wa nchi za AU uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sipopo,jijini Malabo,Equatorial Guinea leo asubuhi.Hotuba hiyo ya kusisimua ilitilia mkazo kwa nchi za Afrika kushirikiana ili kujiletea maendeleo na kuepuka misaada yenye masharti inayolididimiza bara la Afrika katika lindi la umaskini.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Umoja wa Afrika unaofanyika jijini Malabo, Equatorial Guinea(picha na Freddy Maro)


MAMBO YA SABASABA

Wakazi wa Jiji wakiangalia jinsi Mjasiriamali, Anjela John anavyofuma nguo kwa kutumia mashine ya asili jana katika banda la Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kwenye maonesho hayo jana.

Balozi wa Irelanda, Fullam akiaangalia vyombo vya asili katika moja ya mabanda ya wajasiriamali, katika maonesho ya Biashara.

YANGA YAITUNGUA ELMAN YA SOMALIA 2-0

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kwanza dhidi ya Elman ya Somalia katika michuano ya Kagame Castle Cup kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Picha zote na Kamanda Mwaikenda.

Keneth Asamoah (katikati) wa Yanga, akiwanyanyasa wachezaji wa Elman ya Somalia katika michuano ya Kagame Castle Cup, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda mabao 2-0.Mashabiki wa Yanga wakishuhudia pambano hilo


Mambo yalikuwa hivi

Nurdin Bakari wa Yanga akiwakusanya wachezaji wa Elman ya Somalia


MAKATIBU 6 WA MIKOA WAONDOLEWA CCM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewaondoa makatibu wake wa mikoa zaidi ya sita nchini ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wake wa kujivua gamba ulioanzishwa mapema mwaka huu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wahariri wa magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), alipofanya ziara katika makao makuu ya kampuni hiyo Tabata-Relini jijini Dar es Salaam.
MCL ndiyo inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.Katika ziara hiyo, Nape alisema kuwa zoezi hilo la kuwaondoa makatibu litaendelea hadi ngazi ya makatibu wa wilaya ikiwa ni sehemu ya falsafa ya CCM ya kujivua gamba.
Alisema kujivua gamba ni dhana pana ambayo msingi wake ni kufanya mabadiliko ya kiutendaji na uendeshaji wa CCM kwa ujumla wake na kwamba yapo mambo mengi ambayo yamefanywa katika kutekeleza azma hiyo.
“Makatibu wa mikoa kama sita au saba hivi wameshaondoka na wengine wamestaafu, ni katika kujivua gamba na tutaenda kwenye wilaya pia,”alisema Nape.
Alipoulizwa iwapo hao walioondoka katika nyadhifa zao wamestaafu au wameondolewa, Nape alijibu kwa kifupi “vyote kwa pamoja”.
Alitaja baadhi ya mikoa ambayo makatibu wake wameondolewa kuwa ni pamoja na Shinyanga, Dodoma na Kagera.
Utaratibu wa kumpata mgombea uraisAlisema jambo jingine ambalo linafanyika kupitia mchakato huo ni chama hicho kuangalia upya utaratibu wa kumpata mgombea urais ambao utakuwa tofauti na uliokuwa ukitumika katika chaguzi zilizopita.
“Kuna kamati inashughulikia hilo,” Nape alisema na kuongeza:"Pia tunataka tuwe na kamati kama za Bunge ili kutathimini jinsi Serikali inavyotekeleza ahadi ambazo chama kimezitoa ama kupitia wagombea au kwenye Ilani ya Uchaguzi."
Alisema hatua hiyo itakiwezesha chama hicho kubaini udhaifu uliopo katika utekelezaji wa wajibu wake kwa umma, tofauti na sasa ambapo hakuna mfumo unaowawezesha ufuatiliaji huo.
Nape alisema kuwa hivi sasa wanafanya mabadiliko katika mfumo wa uongozi katika makao makuu ya chama hicho na ndiyo maana hakuna mawaziri katika safu za juu za uongozi.
"Hivi sasa hakuna mawaziri, kwani wakati ule walikuwepo mawaziri katika chama ambao ni viongozi, sasa tupo wenyewe na tunakiendesha chama,"alisema na kuongeza:"Hata mfumo wa ndani katika kitengo changu cha Itikadi na Uenezi nako tunafanya mabadiliko na taarifa zitakuwa zikitolewa in details(kwa undani) na si kwa ufupi ili wananchi wazipate."
Kauli yake kuhusu watuhumiwa ufisadiKuhusu watuhumiwa wa ufisadi na siku 90 walizopewa kujiondoa kwenye nyadhifa wanazoshikilia ndani ya chama, Nape alisema kuwa hakuna suala la siku 90 bali ni vikao vya chama vitakutana na kutoa maamuzi.
"Siku 90 zinazozungumzwa ni tafsiri ya watu pale mwenyekiti wa chama (Jakaya Kikwete) aliposema tutakutana baada ya miezi mitatu na watu wakatafsiri hivyo, lakini vikao vya NEC ndivyo vinatoa maamuzi,"alisema Nape.
Alisema kuwa hadi hivi sasa hajui makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alichozungumza na watuhumiwa hao wa ufisadi baada ya kukutana nao.
"Sikuwepo kwenye kikao hivyo hadi sasa sijui walizungumza nini, na siwezi kwenda kumtaka Katibu Mkuu anieleze kilichozungumzwa kwani katika vikao vijavyo tutapata taarifa,"alisema Nape.
CCM na vijanaNape ambaye alizungumzia mambo mbalimbali ya chama na Serikali alisema kuwa hali ya CCM kuwasahau vijana iliwaletea matatizo katika Uchaguzi Mkuu uliopita na ndiyo maana hivi sasa chama hicho kimeamua kujivua gamba.
Aliwaasa vijana walioko vyuoni kwa sasa akisema kuwa siyo vizuri kwao kudhani kuwa siasa ni ajira na kwamba endapo kila mwanafunzi atafikiria hivyo, hali hiyo haitawasaidia kitu.
Kuhusu takwimu za Serikali na ndani ya CCM, Nape alisema kuwa kuna ugonjwa mkubwa katika utoaji takwimu kwa kuwa takwimu nyingi zimekuwa ni za uongo.
“Udanganyifu wa takwimu unakuwa kama ni tabia na ipo kwenye chama na kwa Serikali,”alisema.
Alisema katika kila jimbo takwimu zao zinaonyesha asilimia 70 hadi 80 ya watu ni wanaCCM, lakini inashangaza kwa nini wanapata ushindi wa chini kwenye uchaguzi.
Wananchi wana haki ya kupata habariAlisema kuwa atakuwa tayari kuwasaidia wanahabari kupata taarifa za serikalini ambazo zinakaliwa na maafisa habari au watu wa serikalini kwa kuwa wananchi wana haki ya kupata taarifa kuhusu Serikali yao.
“Kama kuna taarifa mnaihitaji serikalini nitawasaidia kuipata ili watu wapate habari kwa kuwa, Serikali ni ya CCM na sisi ndiyo viongozi wa chama,”alisema Nape.
Kuhusu kusherehekea miaka 50 ya Uhuru, Nape alisema kuwa ni vizuri wananchi na wanasiasa wakalinda historia ya taifa kwa kuwa limetoka mbali tangu Uhuru ulipotikana.
“Ombi langu kwa wananchi ni hili, miaka 50 ya Uhuru ni safari ndefu, nataka dhana ya kwamba hakijafanyika chochote iondoke, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilianzia jengo la Ushirika na leo kipo eneo lake halafu mtu anabeza, hilo haiwezekani,”alisema.
Alisema kuwa pamoja na vyombo vya habari kufichua maovu ndani ya nchi, lakini ni lazima vilinde historia ya nchi tangu ilipopata Uhuru.
Akingia kifua gazeti la Mwananchi
Akizungumzia hali ya CCM na Serikali dhidi ya gazeti hili , Nape alisema kuwa fikra ya kwamba chama chake kinaliona gazeti la Mwananchi kama lina mlengo wa chama kingine haipo na ifutike.
“Nimekuja kwa mambo matatu, kufahamiana, kufuta dhana ya CCM kulalamikia magazeti na kutoa msimamo wa chama kuondoa dhana kwamba Mwananchi ina mlengo wa chama kimoja cha siasa,”alisema.
Alisema kuwa ni muhumu CCM ikatambua kuwa gazeti la Mwananchi ni wadau wa mabadiliko katika jamii, hivyo mstari uliopo kati ya CCM na Mwananchi ufutwe.
“CCM kama taasisi tunajua Mwananchi inaaminika na ina wasomaji wengi kuliko gazeti jingine nchini, pia tunajua linaaminiwa na watu na chama pia,” alisema Nape.
Akizungumza kuhusu hilo, Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya MCL, Theophil Makunga alisema kuwa Mwananchi kama gazeti lina sera zake na moja ya sera hizo ni kutoegemea upande mmoja.
Alisema kuwa maamuzi ya habari gani inayofaa kuchapwa kwenye magazeti ya MCL hayafanywi na mtu mmoja bali hupitia vikao vya wahariri vinavyofanyika mara mbili kwa siku.
“Hata editorial (tahariri) haifanywi na mtu mmoja ni uamuzi wa wahariri,”alisema Makunga.
Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

ZITTO;SHIBUDA NI MSALITI, HAAMINIKIKITENDO cha Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (pichani) kupingana na sera ya chama chake kuhusu suala la posho za vikao (sitting allowance), kimeichefua Chadema ambayo imemuita msaliti ikisema, "adhabu yake ni kufukuzwa.
"Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliliambia Mwananchi mjini Dodoma jana kuwa, alikerwa na kauli iliyotolewa na Shibuda ya kwenda kinyume na msimamo kambi hiyo kupinga posho za vikao kwa wabunge na wafanyakazi wengine wa umma.
Mbowe alisema kwamba kwa kauli yake ya juzi ya kuunga mkono posho ilidhihirisha kwamba mbunge huyo ni msaliti wa kambi hiyo, hivyo sheria zitafuata mkondo wake.
"Kutokana na tukio la jana (juzi) bungeni, Shibuda kutusaliti katika suala la posho za vikao, taratibu za kisheria zitafuata mkondo wake kwani utovu wa nidhamu haukubaliki katika kambi yetu, hata katika chama chetu,"alisema Mbowe na kuongeza:
"Suala la posho si la mtu binafsi, lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa 2010 ya chama chetu na kama kuna kiongozi hafahamu hili basi hakustahili kugombea ubunge kwa sababu naamini Ilani ya Uchaguzi, Shibuda anayo."
"Posho zilijadiliwa na kupitishwa katika vikao maalumu vya chama, kwa hiyo kama Katiba yetu ya chama inavyotuongoza, Shibuda alitakiwa kulipinga katika vikao hivyo sio kutoka nje ya kikao na kuanza kupingana na maamuzi yake,"alisema Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema.
Akinukuu kifungu katika Katiba ya chama chake kinachoeleza maadili ya viongozi, Mbowe alisema, "Kiongozi anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa na viongozi wa ngazi ya juu au vikao halali na kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kwa kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye kanuni."
Kauli ya ZittoKwa upande wake, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe, aliliambia gazeti hili jana kuwa mbunge kupingana na sera ya chama chake, ni kutokiamini chama hicho.
"Maana yake hakiamini chama, hivyo hafai kuendelea kuwa mwanachama na mbunge wa chama hicho,"alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.
Aliendelea, "Hapa kuna mambo mawili; masuala ya kisera na masuala ya utaratibu. Mbunge anayepingana na taratibu adhabu yake ni kumwita na kumpa onyo, lakini mbunge anayepingana na sera, huyo hakiamini chama na dhabu yake ni kufukuzwa."
Kwa mujibu wa Zitto, suala la kupinga posho kwa Chadema ni sera kwa kuwa limo kwenye Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2010.
"Hili (suala la posho), lipo kisera. Kwenye Ilani yetu ya uchaguzi tulisema, tutapunguza mishahara ya wabunge na posho zao. Sasa kama mbunge anachaguliwa kwa sera hiyo halafu anaipinga haradhani, huyo hakiamini chama na chama hakipaswi kumwamini."
Aliendelea,"Sasa, adhabu ya juu kabisa ya mbunge asiyekiamini chama, ni kufukuzwa. Huu ni usaliti. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mwenyekiti wa chama ameshalitolea tamko suala hilo halafu mbunge anakuja kumpinga hadharani maana yake nini,?" alihoji.
Tundu Lissu je?Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema kitendo cha Shibuda kupingana na sera ya chama chake, "ni uasi usiovumilika".
"Sasa nikiwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni nadhani ninahitaji kukaa naye. Nitamwita anieleze kulikoni. Aseme kulikoni ameamua kukiasi chama na upinzani kwa ujumla?"
Aliendelea, "Lakini kwa bahati mbaya sana, adhabu kubwa inayoweza kutolewa na kambi ya upinzani ni kumtenga na kambi. Lakini kwa mtu kama Shibuda ambaye tayari anaijua adhabu hiyo na kuitafuta kwa makusudi, inaonekana haitamtosha."
"Kwa sababu hiyo basi, kambi ya upinzani itaenda mbali zaidi baada ya kumtenga. Tutakiandikia chama barua kukijulisha usaliti huo wa mbunge wake halafu chenyewe kina taratibu zake za kinidhamu."
Kauli ya ShibudaJuzi alipokuwa akichangia Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2011/2012, Shibuda alitoa mpya pale alipopingana na misimamo wa Chadema kuhusu malipo ya posho kwa wabunge na watumishi wengine wa umma.
Akitumia lugha yake ya mashairi, Shibuda aliliambia Bunge kuwa utata uligubika posho za wabunge na watumishi wengine wa umma, unatokana na tafsiri potofu ya neno hilo ambalo asili yake ni Ujira wa Mwia.
"Ujira wa Mwia (sasa posho) yalikuwa malipo anayopewa mtu kwa kazi anayoifanya ili kumwongezea hamasa ya kuendelea kuifanya kazi hiyo. Kwa bahati mbaya sasa neno hilo linaitwa posho na ndiyo sababu linaleta mjadala bungeni,"alisema Shibuda huko akishangiliwa na wabunge wa CCM.
Kwa mujibu Shibuda, kama maana ya posho ni Ujira wa Mwia kama ilivyokuwa ikitumika na wakoloni, haina sababu kuifuta kwa kuwa ndiyo hamasa kwa wabunge na watumishi wengine wa umma kuendelea kufanya kazi yao.
Shibuda alilitahadharisha Bunge kuwa mjadala wa posho umetokana na Bunge kuwa na aina mbili ya wabunge; wabunge maslahi jamii na wabunge maslahi binafsi.
"Wabunge maslahi binafsi hawashiriki misiba, hawatembelei hospitali wakasaidia dawa, hawaendi kwenye sherehe na hawana msaada wowote kwa jamii. Sasa aina hiyo ya wabunge hatutegemei kwa nini watake posho,"alisema
Aliendelea,"tabia ya choyo ndiyo inayowasumbua wabunge hao. Lakini pia tujue kwamba kuna wabunge wafanyabiashara na wabunge maslahi, mbunge maskini hawezi kuacha kuchukua posho, sasa ni vema tukatambua tofauti hizo ili tumalize mjadala huo."
Shibuda alipendekeza posho ziendelee kutolewa tena kwa haraka zaidi na nyongeza kubwa badala ya kuendelea kuvutana kuhusu uhalali wake nje na ndani ya Bunge.
"Mheshimiwa Spika, posho haitoshi, inafaa kuongezwa hadi Sh500,000. Mimi nasema na kazi ya kutafsiri ninachosema inategemea busara ya mtu, lakini posho ziongezwe ili zisaidie wabunge maskini, shughuli mbalimbali za kijamii."
Wakati Shibuda akiwa anaeleza hayo, Mbowe, alionekana akitikisa kichwa kwenye kiti chake.
Msimamo wakeLakini Shibuda alilimbia gazeti hili jana atashangaa kama atatuhumiwa kwa maoni yake binafsi aliyoyatoa bungeni juzi juu ya kutaka wabunge waendelee kulipwa posho za vikao vya Bunge.
"Nitashangaa kama nitaitwa na kiongozi yoyote wa kambi yetu ya upinzani au Chadema kwa tuhuma za kutoa maoni yangu huru niliyoyatoa bungeni jana (juzi), hata nilipokuwa CCM nilipenda kusahihisha palipokuwa na makosa".
"Sitarajii Chadema kuna viongozi wanaweza kudidimiza demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, wakati chama kinafanya maandamano kutoa maoni huru kwa Watanzania. Kama mimi sitakiwi kutoa maoni huru basi hakuna maana ya kuandamana kutoa maoni kwa Watanzania".
"Tusitafute hila na visa kwa maslahi binafsi, tutambue kwamba mbunge anapozungumza bungeni anasema kwa maana pana kwa watu wenye mitazamo tofauti kwa lengo la kuleta fikra endelevu".
Alisema kwamba hana habari kama wabunge wote wa Chadema walikutana na kukubaliana kuikataa posho ya vikao vya Bunge.
Shibuda akifafanua zaidi suala hilo la posho japo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa 2010 ya chama chake ilitaka kupunguza posho hizo za vikao pamoja na mshahara wa mbunge, alisema, "Ilani ya Uchaguzi ni mpango kazi wa kuendeleza programu ya chama kilichopo madarakani, kwa hiyo hivi sasa hapa bungeni bila kujali itikadi zetu wabunge tunaunganishwa na programu ya kuendeleza nchi, utawala bora na uongozi wa kuongoza fikra za Watanzania".

KITNE;UTAJIRI WA WACHAHE TZ NI HATARIMkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa katika Serikali ya awamu ya kwanza Dk Hassy Kitine, akizungumza Dar es Salaam jana na washindi wa shindano la shinda 'Nina Ndoto' linaloendeshwa na Kampuni ya Faidika. Picha na Emmanuel Herman ]
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa katika Serikali ya awamu ya kwanza Dk Hassy Kitine, akizungumza Dar es Salaam jana na washindi wa shindano la shinda 'Nina Ndoto' linaloendeshwa na Kampuni ya Faidika. Picha na Emmanuel HermanMwandishi WetuALIYEWAHI kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa katika Serikali ya awamu ya kwanza Dk Hassy Kitine amesema hali iliyopo sasa nchini ya umaskini mkubwa kwa wananchi inatishia amani.
Kitine ambaye aliwahi pia kuwa mbunge amesema taifa haliwezi kuwa na asilimia moja pekee ya watu wanaoshikilia uchumi wa nchi kama ilivyo sasa Tanzania huku asilimia 99 wakiwa mafukara.
"Watanzania wengi ambao ndiyo wenye nchi hii wanamiliki uchumi kwa asilimia moja tu, huku Watanzania walio chini ya asilimia moja kwa wingi wao wakimiliki uchumi kwa asilimia 99,"alisema Kitine na kuongeza:
“Hali hii inatisha na ni hatari kwa kundi dogo la watu wachache kumiliki uchumi wa Watanzia kwa asilimia 99.“
Mbele ya wanahabari Kitine alisema, "Mnajua napenda kusema, lakini nikisema wengine wanakasirika. Lakini, lazima tusema, Watanzania wengi lazima wamiliki uchumi kikamilifu na si watu wachache."
Akijibu swali kuhusu maandamano yanayoendeshwa na Chadema kupinga hali ngumu ya maisha nchini alisema anakiunga mkono chama hicho akisema kiko sahihi katika kufanya maandamano hayo.
"Hali hiyo ni kitu ambacho kizuri na kinaleta changamoto kwa ‘political parties’ (Vyama vya siasa) na viongozi, kwani hawawezi kufanana, maandamano ni mazuri, ni demokrasia, japo mimi ni mwanachama wa CCM," alisema Kitine.Akizungumzia Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na kipindi cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya Nne ya Jakaya Kikwete, Kitine alisema kwamba haoni tofauti katika vipindi hivyo viwili.Hata hivyo, alisema mambo yamekuwa mabaya kutokana na kuondolewa kwa Azimio la Arusha na kwamba uongozi sasa umekuwa wa kununua."Zamani nilipokuwa kiongozi katika Serikali ya Awamu ya Kwanza baada ya kuteuliwa na Rais Nyerere kushika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Uwaziri na hatimaye Ubunge, uongozi ulikuwa ni ‘dedication’,"alisema.
Alifafanua, "zamani ukitaka kugombea nafasi ya uongozi kama ubunge unaulizwa mali umepata wapi, wenzako wataakuuliza, lakini nikaacha kugombea tena uongozi kutokana hali iliyojitokeza ambayo sasa uongozi unanunuliwa."
Kuhusu kampuni yake ya Faidika amesema hivi sasa inajishugulisha na kuwasaidia wafanyakazi wa sekta ya umma na hapo baadaye itaanza kusaidia pia watu wa sekta binafsi .
Kitime alikuwa akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la pili la ‘shinda ndoto yako’ linaloendeshwa na Kampuni ya Faidika inayojishugulisha na mikopo kwa wafanyakazi wa umma.
Kuhusu kampuni ya Faidika alisema hivi sasa inajishugulisha na kuwasaidia wafanyakazi wa sekta ya umma na hapo baadaye itaanza kusaidia pia watu wa sekta binafsi .
Katika hafla ya jana Mwalimu ya Shule ya Msingi Pongwe iliyopo mkoani Tanga Amiri Ligalwike alikabidhiwa Sh 5 milioni baada ya kuandika mchanganua wake vizuri kuhusu fedha alizokopa sh1.5 milioni jinsi alivyozitumia na kuweza kuboresha maisha yake ya kila siku na jirani zake.Mshindi mwingine ni Makono Andrew aliyeshinda Sh 3 milioni.

TWIGA KWENDA ZIMBABWE

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuondoka Julai Mosi mwaka huu kwenda Harare, Zimbabwe kushiriki mashindano ya COSAFA yanayoanza Julai 2 mwaka huu jijini humo. Twiga Stars inayofundishwa na Kocha Charles Boniface akisaidiwa na Nasra Mohamed itaondoka saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ikiwa na msafara wa watu 26. Katika msafara huo wachezaji ni 19 huku benchi la ufundi likiwa watu wanne. Kiongozi wa msafara ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) Lina Mhando ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Twiga Stars inashiriki michuano hiyo ya Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) ikiwa timu mwalikwa. Jumla ya timu nane zinashiriki wakiwemo wenyeji Zimbabwe. Nyingine ni Lesotho, Botswana, Afrika Kusini, Zambia, Msumbiji na Malawi. Twiga ambayo iko kundi A pamoja na Zimbabwe, Lesotho na Botswana itacheza mechi yake ya kwanza Julai 2 mwaka huu dhidi ya Botswana kwenye Uwanja wa Gwanzura.
Siku inayofuata itacheza na Lesotho kwenye Uwanja wa Rufaro kabla ya kumaliza mechi za makundi Julai 5 mwaka huu kwa mechi dhidi ya wenyeji kwenye Uwanja wa Gwanzura. Hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo itafanyika Julai 7 mwaka huu. Kila kundi linatoa timu mbili kuingia katika hatua hiyo na nusu fainali zote pamoja na fainali zitachezwa Uwanja wa Rufaro. Boniface WamburaOfisa Habari

Cole: Mchezaji bora wa dunia atoke Tanzania

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United ya England, Andy Cole amezindua programu ya kuendeleza vipaji vya soka kwa watoto chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars na kuwataka Watanzania kuitumia programu hiyo ili siku moja iweze kuitangaza Tanzania.

Mchezaji huyo alisema kuwa pamoja na kuzindua program hiyo, anataka siku moja kuona mchezaji wa Tanzania anakuwa mwanasoka bora wa Dunia.

Program hiyo ilizinduliwa kwa ushirikiano wa klabu ya Manchester na Kampuni ya Simu ya Airtel ambayo itafanyika katika ngazi ya Mikoa na Taifa na kuhitimishwa kwa Kliniki ya Soka itakayofanyika nchini Gabon na Tanzania chini ya Usimamizi wa Jopo la makocha kutoka Manchester United.
Akizungumza katika uzinduzi wa programu hiyo iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Makongo, Cole alisema: "Michezo ni sehemu ya maisha, nina imani Tanzania ikiwekeza katika michezo itafika mbali kimataifa na siku moja mchezaji bora wa Dunia atatoka Tanzania.

"Nimekuja Tanzania kwa ajili ya michezo naomba Watanzania watoe sapoti kwa vijana hawa wadogo ambao siku moja wataleta mapinduzi katika Soka la Afrika na hasa Tanzania," alisema Cole.

Mwakilishi wa Klabu ya Manchester United ambaye aliongozana na Cole katika uzinduzi huo, Nick Hamfrey alisema Watanzania wanatakiwa kutumia nafasi hii katika kuendeleza vipaji vya watoto kwani soka inahitaji maarifa na nia ya dhati ndani na nje ya uwanja.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangallor alisema program hiyo itatoa fursa kwa vijana hao kuonyesha uwezo wao mbele ya mawakala wa Soka, Makocha sambamba na kupata fursa ya kujiendeleza zaidi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara alisema programu hiyo itaongeza msukumo katika mpango wa maendeleo ya soka nchini kwa sababu vijana wa Tanzania watapata msaada wa kitaalamu kutoka katika timu maarufu duniani.

Naye Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Leodegar Tenga alisema miradi yenye lengo la kuibua vipaji na kuviendeleza ni muhimu kwa maendeleo ya soka hapa nchini na kuwataka Airtel kuwa bega kwa bega na klabu hiyo ya Manchester katika kuendeleza soka la Tanzania.

Andy Cole,39, hivi sasa anafanya kazi katika kituo cha mazoezi cha Manchester United kilichopo huko Callington huku akimalizia kozi yake ya ukocha, lakini kabla ya hapo alikuwa kocha wa washambuliaji katika klabu ya Huddersfield inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini England.
Cole alistaafu soka 2008 baada ya kuzitumikia klabu za Bristol City, Newcastle United, Manchester United, Blackburn Rovers, Fulham, Manchester City, Portsmouth, Birmingham City, Sunderland , Burnley na Nottingham Forest na kufunga mabao 187 katika Ligi Kuu ya England.

ANDY CORE WA MAN U ATUA NCHINI

Mchezaji wa zamani wa Manchester United ya Uingereza, Andy Core (katikati) waliosiosimama) akiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Makongo, Dar es Salaam,wakati wa uzinduzi wa vijana wenye vipaji vya kucheza soka. Core ni mwenyeji wa kampuni ya simu ya Airtel.
Andy Core akisalimiana na Naibu Waziri wa Habari, Vijana na Michezo, Dk. Mukangara walipokutana wakati wa uzinduzi huo. Katikati ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetilleh Osiah.

SIMBA MBABE WA OCEAN VIEW

Wachezaji wa Simba wakishangia bao la kuongoza dhidi ya Zanzibar Ocean view jioni ya leo katika mtanange wa kugombea kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

WAREMBO WALIOINGIA MISS REDDS KANDA

Meneja wa kinywaji cha Redd's Premium Cold, Victoria Kimaro (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya warembo walioshinda katika mashindano ya urembo ya vitongoji na kufanikiwa kuingia michuano wa kanda inayodhaminiwa na kinywaji hicho. Kimaro alifanya mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, ambapo alitangaza kuanza kwa mashindano hayo ya kanda. Kutoka kushoto ni Faiza Ali, Naomi Jones, Stellah Mbuge,Mwajabu Juma na Cynthia Kimasha. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

PINDA NA SIMBAKALIA BUNGENI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Simbakalia kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 29, 2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

AJALI YA DALADALA YAUA MMOJA DAR

Daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Temeke, Dk.Richard Msunga (kushoto)

na Dk. Kuwendwa, wakitoa huduma ya kwanza kwa abiria Mohammed

Ngwale aliyejeruhiwa katika ajali ya daladala namba T 241 AZB,

iliyogongana na Lori namba T 504 AWH Dar es Salaam, katika makutano

ya barabara za Mandela na Kilwa. Hata hivyo majeruhi huyo alifariki

baadaye.(PICHA
Mmoja wa vijana aliyejeruhiwa
Msichana aliyeruhiwa kwenye ajali hiyio akisubiri tiba katika Hospitali ya Temeke
Baadhi ya majeruhi wakipelekwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu

JK USO KWA USO NA BILL GATES IKULU DAR


President Dr. Jakaya Kikwete (2nd-L) and Vice President, Dr. Mohammed Gharib Bilal, in a group photo with the Chairman of Bill and Melinda Gates Foundation, Bill Gates (L) and his wife, Melinda gates, who is the Co-Chair, shortly after the president had talks with him at State House in Dar es Salaam Wednesday June 29, 2011. (Photo; State House)

Mwenyekiti mwenza wa Taasisi ya Bill na Melinda Gates, Bill Gates (kushoto) kutoka Marekani, akizungumza na Rais Jakaya Kikwete, alipowasili Ikulu, Dar es Salaam . (PICHA YA IKULU)

TIGO IMEJIPANGA KWELI KWELI SABASABA

Wasichana waliopata ajira ya muda kwenye Banda la Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, wakiwa na vipeperushi walivyokuwa wakivigawa kwa watu waliojitokeza kwenye viwanja vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.

Bango likionesha picha za mawaziri waliowahi kuongoza Wizara ya Maliasili ya Utalii tangu 1961 mpaka sasa.Bango hilo lipo kwenye banda la wizara hiyo katika maonesho hayo.WALANGUZI WA VIWANJA VYA WAZI KINONDONI WAFIKISHWA KIZIMBANI

Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wa Manispaa ya Kinondoni, wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, ambapo walisomewa mashitaka 45 ya kutoa taarifa za uongo na kutumia vibaya madaraka yao na kujipatia ardhi kinyume cha sheria

MAFUTA SASA KUAGIZWA KWA MKUPUO

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu akizungumza katika mkutano na wadau wa uuzaji wa mafuta ya petroli nchini, Dar es Salaam, kuhusu utaratibu mpya uliowekwa na Serikali wa kuagiza mafuta kwa pamoja ili kudhibiti upandaji holela wa nishati hiyo.

MAMBO YA BUNGENI

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiteta na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lymo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Maombo ya Ndani, Shamsi Nahodha, Bunge mjini DodomaLIBYA YAPUUZA HATI DHIDI YA GADDAFFI

Kanali Muammar Gaddafi

Waziri wa sheria nchini Libya Mohammed al Qamoodi amesema hati za mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita za kutaka Kanali Muammar Gaddafi akamatwe zimelenga kuficha uhalifu wa Nato.

Akizungumuza mjini Tripoli, Bw Qamoodi amesema operesheni za Nato zinazoendelea nchini humo ni uhalifu wa kivita dhidi ya raia wa Libya lakini ICC imezifungia jicho.
Waziri huyo ameongeza kuwa wanajeshi wa Nato sasa wamepata kisingizio cha kumuua kiongozi wao Kanali Gaddafi.
Hata hivyo ametangaza kuwa Libya imepata fursa ya kufungulia Nato mashtaka ya uhalifu wanaoendeleza nchini Libya.
Mahakama hiyo imemtuhumu Gaddafi kwa uhalifu dhidi ya binadamu na kuamuru mashambulio kwa raia baada ya machafuko dhidi yake kuanza kati kati ya mwezi Februari.
Mahakama hiyo iliyopo the Hague pia imetoa hati ya kukamatwa kwa mtoto wake wa kiume Saif al-Islam na mkuu wa idara ya ujasusi Abdullah al-Sanussi.
Hatua hio imeendelea kuzua hisia tofauti.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Urusi, Konstatin Kosachev amesema kuwa uamuzi wa jaji hao sasa utavuruga juhudi za kutafuta suluhu ya mzozo huo.
Bw Kosachev amesema nia kuu ya jumuiya ya kimtaifa ni kuwa Kanali Gaddafi ajiuzulu na atoke nchini humo lakini sasa hilo huenda lisifanyike.
Badala yake, Kosachev amesema huenda kiongozi huyo atafanya kila juhudi kushinda vita hivyo na hii sio habari njema kwa Libya.
Lakini kwa upande wao, wapinzani wamekaribisha uamuzi huo.
Msemaji wao Ibrahim Dabbashi amesema sasa jukumu lipo kwa washirika wa Gaddafi kuelewa kuwa wanafanya kazi na mhalifu na wamshauri aondoke madarakani.
Maelfu ya watu wanaaminiwa kufariki dunia kwenye ghasia hizo.

BARAZ\A LA KRIKET ULIMWENGUNI KUTOPUNGUZA TIMU

Timu ya Kenya

Baraza la mchezo wa kriketi ulimwenguni ICC latangaza kwamba limeamua kutupilia mbali hatua ya kuzipunguza timu katika Kombe la Dunia 2015Mataifa kama Kenya, Ireland na Canada, huenda yakanufaika tena kufuatia hatua ya baraza la kriketi ulimwenguni, ICC, kuamua kutupilia mbali wazo la kupunguza timu zitakazoshiriki katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2015, hadi timu 10 tu.
Mwezi Aprili, baraza la ICC lilikuwa limetangaza nia ya kuzipunguza timu hadi 10, kuyaruhusu mataifa wanachama kamili peke yao kupambana katika mashindano hayo.
Baadhi ya wadadi wanasema timu kama Kenya hazipati msaada wa ICC kushirikishwa katika mashindano makubwaIkiwa hatua hiyo ingelitekelezwa, mataifa kama Kenya na Zimbabwe yasingeliweza kushiriki.
Lakini wakuu wa kamati kuu ya mchezo huo ambao wanaendelea na kikao chao cha kila mwaka, wamekubali mashindano hayo yaendelee kuwa na timu 14.
Hayo yanamaanisha kuna mataifa manne ambayo yatajiunga na India, Pakistan, Sri Lanka, Uingereza, Afrika Kusini, New Zealand, Australia, West Indies, Bangladesh na Zimbabwe katika mashindano ya mwaka 2015.
Mbali na Ireland, ambao waliweza kuishinda England katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2011, na Pakistan yale ya mwaka 2007, mataifa mengine yasiyokuwa wanachama kamili na yaliyofuzu kushiriki katika mashindano ya mwaka 2011 ilikuwa ni Kenya, Canada na Uholanzi.
Uskochi, ambao walikuwa katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1999 na 2007, walikubali bila ubishi uamuzi wa ICC wa mwezi Aprili kuzipunguza timu hadi 10, lakini walielezea inafaa kuwe na utaratibu fulani wa kuyafanya mataifa yasiyo wanachama kamili kupambana kabla ya kufuzu kushirikishwa katika Kombe la Dunia.
Wazo la kuwa na timu 12 lilijadiliwa katika kamati kuu ya uongozi ya ICC mjini Mumbai, India, mwezi Aprili, lakini wakati huo iliamua kushikilia kwamba timu 10 ni bora.
Wakati huo, aliyekuwa nahodha wa timu ya England, Michael Vaughan, pia alisema ni wazo zuri kuwa na mashindano ya kufuzu.
"Ningelipenda kuona mashindano ya awali ya kufuzu, na mataifa kama Bangladesh na Zimbabwe yakicheza na mataifa kama Ireland, Canada na Kenya na timu za mataifa mengine na timu mbili bora zaidi zikifuzu kwa Kombe la Dunia," alielezea Vaughan.
Lakini licha ya uamuzi huo kuhusiana na mashindano ya mwaka 2015, ICC imethibitisha kwamba mashindano ya mwaka 2019 yatakuwa na timu 10, na 8 zikiwa ndio zinazoongoza katika orodha ya timu bora zaidi kulingana na ICC, na zilizosalia mbili zikiamuliwa kupitia mashindano fulani wa kufuzu.
Kamati kuu ya ICC pia iliidhinisha kuanzishwa kwa utaratibu wa kuzipandisha daraja timu, au kuzishukisha, kama ilivyokuwa imekubaliana juu ya pendekezo hilo hapo awali.
Kamati pia imethibitisha kwamba mashindano ya dunia ya Twenty20 ya mwaka 2012 na 2014 yatakuwa na jumla ya timu 12 (10 za wanachama kamili na mbili za timu zisizokuwa za wanachama kikamilifu).
Huu ndio umekuwa utaratibu wa mashindano hayo tangu yalipoanzishwa mwaka 2007.

CHIPUKIZI BURUNDI ASHIRIKI MICHUANO YA TENNIS YA WIMBLEDONHassan Ndayishimiye (pichani) aandikisha historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa tennis kutoka Burundi kucheza Wimbledon


Mchezaji tennis chipukizi kutoka Burundi, Hassan Ndayishimie, leo amefanikiwa kuandikisha historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza kutoka taifa hilo kushiriki katika mashindano ya Wimbledon.
Lakini Ndayishimiye sio tu alionyesha nia ya kushiriki, bali aliweza pia kumshinda mpinzani wake Matias Sborowitz kutoka Uchina.,
Ameandikisha historia WimbledonAlipata ushindi wa 6-6 6-4.
Ndayishimiye alishiriki katika pambano la vijana wa umri mdogo la mchezaji mmoja kwa mmoja, yaani singles.
Kati ya mapambano mengine ambayo yalitazamiwa katika uwanja wa 17 wa Wimbledon ni pambano la mchezaji mwingine pia kutoka Afrika, Ons Jabeur, ambaye ni raia wa Tunisia, na aliyetazamiwa kucheza na Risa Ozaki kutoka Japan.

SENEGAL WAANDAMANA KUPINGA MGAWO WA UMEME

Maandamano yamezuka katika mji mkuu wa Senegal, Dakar na katika jiji la kusini la Mbour kutokana na ukosefu wa umeme. Jijini Dakar, majengo kadhaa ya serikali yalichomwa moto, zikiwemo ofisi za shirika la umeme la serikali - Senelec.
Majeshi ya usalama katika mji wa Mbour yalipiga mabomu ya machozi kutawanya maelfu ya waandamanaji.
Tatizo la ukataji umeme, ambao umedumu kwa saa 48 katika maeneo kadhaa, limekuja wiki moja tu baada ya kutokea maandamano dhidi ya rais.
"Mamia ya vijana walivamia ofisi za Senelec na kuzichoma moto," amesema mkazi mmmoja wa Dakar, Ismail Diop akikaririwa na Reuters.
Chupa zilizovunjwa, mabaki ya majengo na matairi yaliyochomwa moto vimetapakaa mitaani, amesema mkazi huyo.
Miaka mingi
Mjini Mbour, karibu kilomita 80 kusini mashariki mwa Dakar, ofisi za shirika la umeme pia zilishambuliwa. watu walioshuhudia walisema ofisi za Senelec zilivunjwa na magari yaliyoegeshwa nje kushambuliwa pia.
Senelec imeshindwa kutoa huduma ya umeme ya kuridhisha kwa miaka mingi.
Wiki iliyopita, kulikuwa na maandamano mjini Dakar, yaliyotokana na pendekezo la rais Abdoulaye Wade kutaka kubadilisha katiba.
Maandamano hayo yalikuwa ya kiwango ambacho hakijawahi kuonekana katika kipindi cha miaka 11 ya utawala wa Bw Wade.
Gharama za maisha
Rais huyo alitaka kupunguza kiwango cha asilimia kinachohitajia kushinda urais kutoka asilimia 50 hadi 25 ili kuepuka duru ya pili katika uchaguzi.
Wakosoaji wamesema marekebisho hayo ya katiba yamelenga kuhakikisha Rais Wade, ambaye ana umri wa miaka 85, anachaguliwa tena mwakani.
Bw Wade alingia madarakani katika uchaguzi wa kidemokrasia, lakini sasa anakabiliwa na ongezeko la hasira kutoka kwa wananchi kutokana na matatizo ya umeme ya kila siku na kupanda kwa gharama za maisha.

WATZ WATATU NA WARWANDA WATATU KIZIMBANI KWA MAUAJI AFRIKA KUSINI

Rais Paul Kagame

Lt.Gen.Kayumba Nyamwasa

Raia watatu wa Rwanda Watanzania watatu wamefikishwa kizimbani kwa tuhuma za jaribio la kumuua Lt.Generali Kayumba Nyamwasa.
Alipigwa risasi katika uti wa mgongo wakati akirejeshwa nyumbani akiwa ndani ya gari mwezi juni mwaka jana lakini alinusurika.
Katika tukio lililosababisha mahusiano baina ya Rwanda na Afrika kusini kudorora, upande wa mashtaka unadai kuwa mmoja wa wanaume aliye kizimbani anamfahamu Bw.Nyamwasa.
Dereva wake, Richard Bachisha, ameondolewa kwenye orodha ya washukiwa kwa sababu licha ya kumfahamu Bw.Nyamwasa, aliwahi kufanya kazi chini ya mkuu huyo nchini Rwanda na baadaye kuwa dereva wake nchini Afrika kusini. Wakati wa tukio yeye ndiye aliyekuwa akiendesha gari.
Vilevile kuna mfanyabiashara aliyetajwa kama kiongozi wa mkumbo huo. Yeye alijaribu kuwahonga polisi wa nchi hiyo dola milioni moja wakati akijaribu kupita uwanja wa ndege wa Oliver TAMBO.
Rwanda inamshutumu Bw.Nyamwasa kwa matukio kadhaa ya milipuko mjini Kigali huku Mamlaka za Uhispania na Ufaransa zikidai zinamsaka kuhusiana na uhalifu wa kivita katikati ya miaka ya 90.

Gavana wa benki kuu Afghanistan ajiuzulu

Gavana wa benki kuu nchini Afghanistan Abdul Qadeer Fitrat amejiuzulu kutoka wadhifa huo akihofia maisha yake.
Rais Karzai analaumu washauri wa kigeni kwa hasara iliotokea kwenye benki ya KabulBw Fitrat amsema vigogo serikalini wanamzuia kufanya uchunguzi kuhusu ubadhirifu wa dola nusu bilioni kutoka benki ya Kabul.
Lakini msemaji wa Rais Hamid Karzai, ametaja hatua ya gavana huyo kuwa uhaini mkubwa.
Waheed Omar amesema kuwa uchunguzi ulikuwa umeanzishwa kuhusu utenda kazi wa gavana huyo wa benki kuu.
Uchunguzi umeonyesha kuwa benki hiyo ilitoa mikopo ya mamilioni ya dola bila kufuata maadili, hali iliotishia kuifilisi benki hiyo.
Serikali ya Afghanistan mwaka jana ililazimika kutumia pesa zake kuinusuru benki hiyo.
Rais Karzai aliahidi kuwa uchunguzi utafanyika kuhusu sakata hiyo ya ufujaji wa pesa katika benki hiyo na hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika wote.
Bw Fitrat ambaye sasa yuko uhamishoni, anasema alikuwa na matumaini kuwa uchunguzi huo ungefichua wahusika kwenye sakata hiyo lakini badala yake umechochea matatiza maishani mwake.
"Maisha yangu sasa yamo hatarini. Hii ni baada nilipozungumza bungeni na kufichua watu ambao walihusika na sakata hiyo katika benki ya Kabul" ameelezea Bw Fitrat.
Baadhi ya watu waliotajwa na gavana huyo kuhusika na kashfa hiyo ni ndugu yake Rais Karzai, Mahmoud Karzai.
Idara ya kuchunguza ufisadi nchini Afghanistan ilifichua kuwa zaidi ya dola milioni 467 zilitolewa na benki hiyo kama mikopo kwa vigogo nchini humo bila kufuata utaratibu.
Lakini Rais Karzai alisema nchi yake haina uzoefu wa kutosha kusimamia benki hiyo na amelaumu washauri wa kigeni kwa hasara hiyo iliotokea.

SHADRACK NSAJIGWA WA STARS, YANGA AOPOA KIFAA

Nahodha wa Taifa Stars na Yanga, Shadrack Nsajigwa akiwa mwenye furaha pamoja na mkewe Jane Mwamasangula katika mnuso wa harusi yao uluiofanyika kwenye ukumbi wa makunti wa JKT Mgulani, Dar es Salaam usiku wa kumkia leo. Walifunga pingu za maisha kwenye Kanisa la Moravian Mburahati jijini jana.


Shadrack Nsajigwa akiwa na mwandani wake Janne


Nsajigwa akiwa na wapambe wao pamoja na baadhi ya marafiki

Ni wakati wa furaha (Picha za blogu ya Jamii)AFADHARI YA JELA

Bwana mmoja nchini Marekani anatarajiwa kwenda jela, baada ya kuingia benki na kutaka kuiba dola moja.
Gazeti la Telegraph limesema Bwana huyo James Richard Verone, aliingia benki na kumwambia mfanyakazi wa benki kuwa amekuja kuiba, na anataka dola moja tu.
Baada ya kutoa madai yake hayo, bwana huyo mwenye umri wa miaka hamsini na tisa, aliketi chini, na kusubiri polisi waje kumkamata.
Mwizi huyo, ambaye hana kazi na anakabiliwa na maradhi, amesema lifanya uhalifu huo, ili akamatwe na kufungwa, kwa kuwa anaamini jela ndio mahala pekee atapata huduma za afya.
"Mimi ni mtu wa busara" amesema bwana James "Nilitaka kuweka wazi kuwa nia yangu sio kuiba pesa, bali nahitaji kupelekwa hospitali".
Bwana huyo, ambaye hakutumia silaha yoyote wakati akifanya wizi hu, amesema ana imani kuwa huenda akapewa hukumu ya kifungo cha miaka mitatu jela, huku akipata huduma za hospitali.
Wizi huo ulitokea katika benki ya RBC, North Carolina

PWEZA WANNE KUSHINDANA UJERUMANI

Pweza wanane nchini Ujerumani watashindanishwa kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la soka kwa wanawake itakayoanza hivi karibuni.
Pweza hao watashindanishwa kutafuta mrithi wa pweza Paul, aliyepata umaarufu wa kutabiri matokeo ya mechi za soka za Kombe la Dunia mwaka jana Afrika Kusini.
"Kwa sasa tunawafanyia mazoezi na mafunzo tukiwa na matumaini ya kupata japo mmoja atakayeweza kutabiri" amesema Britta Analauf, msemaji wa idara inayoandaa michuano ya Kombe la Dunia.
Kila siku kuanzia saa tano kamili asubuhi pweza hao wanane, waliopo katika miji tofauti watakuwa wakipewa mitihani ya kutabiri mambo mbalimbali.
Pweza hao wanatoka miji ya Hanover, Koenigswinter, Konstanz, Minich, Speyer, Timmendorfer Stand, na mji aliotoka Paul, Oberhausen.
Utabiri huo wa mazoezi haujatajwa rasmi, lakini gazeti la Metro limesema itakuwa ikilingana kidogo na kile alichokuwa akifanya Pweza paul mwaka jana, pale alipojizolea sifa za kubashiri sawasawa matokeo ya mechi zote saba za Ujerumani.
Pweza Paul alifariki dunia akiwa na umri wa karibu miaka mitatu, mwezi Oktoba mwaka jana.

SONG APIGWA FAINI

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal, Alex Song (pichani), amepigwa faini na shirikisho la mchezo wa soka nchini Cameroon, kufuatia mzozo uliozuka kati yake na mshambulizi Samuel Eto'o.
Mchezaji wa Cameroon Alex_song
Eto'o hakupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu na kamati kuu ya nidhamu ya shirikisho hilo Fecafoot.
Mchezaji wa Tottenham Hotspurs, Benoit Assou-Ekotto naye alipewa onyo na kamati hiyo ya nidhamu.
Mashtaka dhidi ya wachezaji hao yalihusiana na mchuano wa kufuzu kwa kombe la taifa bingwa barani Afrika dhidi ya Senegal tarehe 4 mwezi Juni na pia katika kambi ya mazoezi kabla ya mechi hiyo.
Song alikataa kumsalimia Eto'o wakati wawili hao walipokutana kabla ya mechi hiyo.
Wawili hao walikuwa wametofautiana wakati fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini na mechi hiyo ilikuwa mechi ya kwanza ya Song tangu fainali hizo na timu hiyo ya taifa.
Song alipigwa faini ya US$2,000 na pia kuamriwa kufanya mazoezi ya siku tatu ya timu ya taifa ya vijana chipukizi mwaka ujao.
Samuel Eto'oEto'o alikabiliwa na mashtaka ya kukosa kufika kambini na pia kumdharau kocha wa timu hiyo Javier Clemente wakati mchezaji huyo alipopinga mabadiliko yaliyotekelezwa na kocha huyo.
Hata hivyo mashtaka hayo dhidi ya Eto'o yalifutiliwa mbali, baada ya uchunguzi kufanyika.
Assou-Ekotto, ambaye hakufika katika kikao cha kamati hiyo, amepewa onyo pia kwa kukosa kuitikia wito wa kufika kambini.
Timu ya Indomitable Lions inakabarua kigumu kufuzu kwa fainali za kombe la taifa bingwa barani Afrika zitakazoandaliwa nchini Equatorial Guinea na Gabon mwaka ujao.
Timu hiyo inashikilia nafasi ya tatu kundi lao alama 5 nyuma na Senegal na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

HATI YATOLEWA KUMKAMATA GADDAFI

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita imetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi (pichani).
Mahakama imemtuhumu kwa uhalifu dhidi ya binadamu na kuamuru mashambulio kwa raia baada ya machafuko dhidi yake kuanza kati kati ya mwezi Februari.
Mahakama hiyo iliyopo the Hague pia imetoa hati ya kukamatwa kwa washirika wake wakuu Kanali Gaddafi- mtoto wake wa kiume Saif al-Islam na mkuu wa kijasusi Abdullah al-Sanussi.
Maelfu ya watu wanaaminiwa kufariki dunia kwenye ghasia hizo.
Hati hizo ziliombwa na mkuu wa mahakama hiyo ya ICC Luis Moreno-Ocampo mwezi Mei, aliyesema watu hao watatu walihusika na "mashambulio yaliyopangwa na yaliyosambaa" kwa raia.
Bw Moreno-Ocampo alisema mahakama hiyo ina ushahidi kuwa Kanali Gaddafi "aliamuru binafsi mashambulio kwa raia wa Libya wasio na silaha na alihusika kwa kukamatwa na kunyanyaswa kwa wapinzani wake wa kisiasa.
Serikali ya Libya hivi karibuni ilisema haitambui mahakama hiyo na tishio la hati hiyo haiwashughulishi.


TRENI SUDANI KUSINI YASHAMBULIWA

Treni katika mji Aweil, Sudan
Treni iliyobeba wananchi wa Sudan Kusini kurudi nyumbani kutoka Kaskazini imeshambuliwa na kundi la Kiarabu kutoka kaskazini na kusababisha kifo cha mtu mmoja, Umoja wa Mataifa umesema.
Msemaji wa Umoja huo alisema treni hiyo ilishambuliwa na kundi la Misseriya wenye silaha katika jimbo la Kordofan Kusini Jumapili ingawa kiongozi wa kundi la Misseriya alikanusha.
Takribani watu 70,000 wameyakimbia mapigano ya hivi karibuni katika jimbo la Kordofan linalopakana na Sudan Kusini.
Wasiwasi umekuwa ukiongezeka huku Kusini ikielekea kupata uhuru wake mwezi ujao.
Watu wengine 100,000 wamelazimika kuyakimbia makazi yao baada ya mapigano katika eneo lenye mzozo la Abyei, karibu na Kordofan Kusini.
Tangu kumalizika kwa vita vya Kusini na Kaskazini miaka 21 iliyopita, Wasudani Kusini wapatao milioni mbili wamerejea nyumbani na wengine zaidi wanaendelea kurudi kabla ya kutangazwa kwa uhuru
wao Julai 9.
"Treni iliyokuwa ikiwasafirisha Wasudani Kusini waliokuwa njiani kutoka Kosti kwenda Wau ilishambuliwa na wapiganaji wa Misseriya," alisema msemaji wa UN Hua Jiang.
Hata hivyo, kiongozi wa Misseriya Mohamed Omer al-Ansary alisema shambulio hilo limefanywa na waasi katika eneo jirani la Darfur, ambako mgogoro tofauti ulitokea mwaka 2003.
Majeshi ya Kaskazini yamekuwa yakilaumiwa kwa kulipua baadhi ya sehemu katika Kordofan Kusini yanayokaliwa na kabila la Wanuba, ambao wamekuwa wakiunga mkono Kusini wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mapigano yalizuka baada ya makundi yanayounga mkono Kusini kuamriwa kunyanga’anywa silaha baada ya Ahmed Haroun kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa karibuni wa ugavana.
Bwana Haroun anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu Darfur.
Mwishoni mwa wiki Bwana Haroun alisema hali sasa ni shwari na watu wameanza kurejea kwenye makazi yao.
Hata hivyo Shirika la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International limeshutumu mamlaka kulazimisha watu kurejea warejee kwenye makazi yao ilhali bado kuna mapigano yanaendelea.


RAIS CHILUBA AZIKWA

Marehemu Fredrick Chiluba na mkewe Regina mjini Lusaka
Aliyekuwa Rais wa Zambia Frederick Chiluba amezikwa kwenye mji mkuu, Lusaka, kufuatia kifo chake wiki moja iliyopita.
Mamia ya waombolezaji, walioongozwa na Rais Rupiah Banda, walihudhuria mazishi hayo.
Bw Chiluba alifariki dunia nyumbani kwake mwishoni mwa juma- sababu ya kifo chake hakijtangazwa kwa umma mpaka sasa.
Aliiongoza Zambia kwenye demokrasia kwa kuanzisha vyama vingi mwaka 1991, lakini urais wake uligubikwa na madai ya rushwa.
Mwandishi wa BBC Mutuna Chanda mjini Lusaka alisema Wazambia wengi wanaamini udhaifu wa Bw Chiluba usiangaliwe sana na badala yake akumbukwe kwa kumaliza utawala wa chama kimoja.
Amezikwa pembeni mwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Levy Mwanawasa, katika makaburi maalum kwa ajili ya Marais.
Bw Mwanawasa, aliyemrithi Bw Chiluba, alifariki dunia mwaka 2008.
Maelfu ya watu walishuhudia mazishi ya Bw Chiluba kupitia televisheni ya taifa na kwenye skrini kubwa ziliozwekwa nchini kote.
Viongozi wakuu kutoka nchi za kigeni waliohudhuria mazishi hayo ni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jospeh Kabila na waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai.


JK ATIA SAINI KUMBUKUMBU YA MAREHEMU FREDERICK CHILUMBA

Rais Jakaya Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya kifo cha Rais wa zamani wa Zambia, marehemu Frederick Chiluba katika Ofisi ya Ubalozi wa Zambia, Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Zambia nchini. Mavis Muyunda. (PICHA NA FREDDY MARO)