Mkuu wa upelelezi mkoa wa Mbeya Anacret Malindisa
aliyehamishiwa Jijini Dar Es Salaa
ASILIMIA 70 za uhalifu na maovu mbalimbali yaliyokuwa
yakiendelea mkoani Mbeya yamedhibitiwa kutokana na jitihada za ushirikiano kati
ya Jeshi la polisi na wadau wakiwemo wazee na viongozi wa
mila.
Hayo yalielezwa juzi na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi mkoa
wa Mbeya Anacret Malindisa aliyehamishiwa Jijini Dar Es Salaa kikazi, katika
hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na Muungano wa jamii
Tanzania(MUJATA).
Alisema Viongozi hao wa mila, kwa kiwango kikubwa
wamesaidia kuwafichua waharifu ambao walikuwa wakifanya maovu katika
jamii.
Alisema ushirikiano alioupata kutoka kwa machifu na
wazee mbalimbali akiwa madarakani ulimsaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na
vitendo vya mauaji yakiwemo uchunaji ngozi,ujambazi na kilimo cha bangi kwa
baadhi ya maeneo ndani ya mkoa na kuufanya mkoa wa mbeya kuwa
shwari.
Mwenyekiti wa Muungano wa Jamii (MUJATA) Shayo Soja
alisema kuwa baada ya kuundwa na kusajiliwa kwa umoja huo mwaka 2009 kumekuwa
na mafakio mengi ya kupambana na maovu mbalimbali katika jamii kutokana na
ushirikiano mkubwa uliopo kati ya wazee,jamii,machifu na wataalam wa jadi
.
Alisema mbali na wadau hao, ushirikiano mzuri uliopo
kati ya MUJATA na jeshi la polisi umefanikisha kukomesha maovu mengi yaliyokuwa
tishio la amani kwa wageni waliokuwa wakitembelea mkoa wa Mbeya pamoja na
wenyeji.
“Tumejitahidi kuibua maovu mbalimbali ambayo mengi
yalishindikana kwa njia ya kawaida hivyo kutokana na kila kundi wakiwemo
wazee,machifu na watalaam wa jadi kushiriki vyema katika kuwafichua waharifu
katika maeneo yao tumefanikisha kwa kiasi kikubwa na ndiyo maana amani ipo
mkoani Mbeya,” alisema Chifu Soja.
Hata hivyo aliwatupia lawama baadhi ya viongozi kwa
kutoungana nao katika kampeni hizo hususani viongozi wa siasa akiwemo Mbunge wa
Jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (CHADEMA) na mbunge wa jimbo la Mbeya
vijijini Mch.Lackson Mwanjale (CCM).
Alisema wabunge hao wameshindwa kujenga ushirikiano wa
karibu na umoja huo katika mapambano dhidi ya matendo maovu katika jamii ili
hali wao ni wawakilishi wa wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa upelelezi Mkoa Mbeya
aliyehamia na kubadili nafasi ya Malindisa, Mwita Chacha ameahidi kushirikiana
na uongozi wa MUJATA katika mapambano dhidi ya matendo maovu ndani ya
jamii.
Alitoa wito kwa wazee,machifu na wataalam wa jadi
kote nchini kujiunga na chama hicho kwa lengo la kufanikisha mapambano dhidi ya
maovu katika jamii ili wafanye kazi nchi
nzima.
|
Comments