BABA AMNYONGA MWANAWE KWA MIKONO

WATU watatu wamefariki dunia katika matukio kadhaa tofauti, likiwamo la baba kumnyonga mwanaye kwa mikono baada ya ugomvi kati yake na mkewe.

Wakati mauaji hayo ya kinyama yakifanyika, watu wengine watatu wamenusurika kufa akiwamo la mke kuchomwa kisu na mumewe kutokana na wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Frasser Kashai alisema katika Kijiji cha Kilemba wilayani Kibondo, baba  alimuua mtoto wake Bahati Kabungu (15) aliyekuwa Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Kilemba kwa kumnyonga shingo hadi kufa.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi usiku wa saa 5:00 usiku baada ya baba huyo aliyekuwa ametoka klabuni kunywa pombe kugombana na mke wake aliyekuwa amebeba mtoto mchanga mgongoni.

Alisema kutokana na purukushani baina ya mke na mume, mtoto aliyekuwa amebebwa mgongoni alidondoka chini na ndipo marehemu Bahati alimwokota na kumbeba.

"Kuona hivyo ndipo baba yake alimwacha mkewe na kumvamia marehemu huyo na kuanza kumnyonga shingo yake hadi kufa," alisema.

Kamanda huyo wa polisi alisema mtuhumiwa alitoroka baada ya kufanya mauaji hayo na kukimbilia kusikojulikana. Alisema juhudi za polisi kumtafuta zinaendelea.

Kamanda Kashai alisema katika tukio lingine juzi, katika Kijiji cha Basanza wilayani Kigoma, kundi la watu waliokuwa na silaha za jadi, walivamia nyumba ya Hussein Matona (48) na kuishambulia nyumba hiyo kwa mawe na kuibomoa kabisa.

ACP Kashai anaeleza kwamba baada ya kuvamiwa, Matona alilazimika kutoka ndani ya nyumba hiyo na kutimua mbio ili kuepuka kuuawa.

Kamanda Kashai alisema katika tukio lingine, mtu mwingine alikutwa amekufa mita kumi kutoka nyumbani kwa Matona. Mtu huyo alikuwa amekatwa  taya la kushoto kwa kitu chenye ncha kali.

Mtu huyo ametambuliwa kwa jina la Windeye Thobias ambaye ni mkazi wa Kijiji hicho cha Basanza.

Mtu mwingine mkazi wa Kijiji cha Kumubanga wilayani Kibondo alikutwa na bunduki ya kivita aina ya SMG yenye namba 1953 – 1995 / 7295 ikiwa na magazini moja isiyokuwa na risasi ndani.

 Matukio yote yamethibitishwa na polisi na uongozi wa hospitali. Matukio hayo yalitokea kati ya Januari 6 na 7, mwaka huu. Mtuhumiwa mmoja ashikiliwa na polisi.

Katika tukio lingine, mtu mmoja anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma kisu mkewe Ghati Marwa Ruhinda (45), mkazi wa Mugumu. Mama huyo alichomwa kisu sehemu ya tumboni.


Akisimulia mkasa huo wifi wa majeruhi huyo Rebeca Ruhinda ambaye anamuuguza alisema tukio hilo lilitokea Januari 7, mwaka huu, saa 1:15 asubuhi katika eneo la darajani wakati wakielekea nyumbani.


Pia polisi wanamsaka mkazi wa kitongoji cha Butiama Kijiji cha Masangura baada ya kudaiwa  kumkata kwa panga mtoto wake sehemu ya kichwani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA