BEI YA MAFUTA YAPANDA

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), imepandisha bei ya mafuta ya Petroli kwa Sh72 zaidi ya ile ya awali.

Mbali na Petroli Ewura imepandisha bei ya mafuta ya Taa kwa Sh5 huku bei ya Dizeli ikibaki kama ilivyo.
Awali bei ya Petroli  iliuzwa Sh1882 na kuanzia leo inatarajia kuuzwa  Sh1954 kwa lita, mafuta ya Taa yaliyouzwa  kwa Sh1958 yatauzwa Sh1963 lakini Dizeli itaendelea kuuzwa Sh1976 kwa lita .

Bei hiyo mpya inayotarajia kuanza kutumika leo kote nchini imekwenda sambamba na kuanza upya kwa matumizi ya  kanuni ya ukokotoaji wa bei za mafuta.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ewura kwa vyombo vya bahari, kanuni hiyo mpya  inakwenda sambamba na kuanza kutumika kwa  kanuni mpya za mfumo wa ukokotoaji wa bei ya mafuta.

“Kanuni hii itaanza kutumika Jumatano ya  Januari 4 mwaka huu,(leo) kwa  Tanzania Bara na itakuwa ikirekebishwa kila baada ya mwezi mmoja” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa ilifafanua kuwa gharama za mafuta zinatokana na ongezeko la  tozo inayotozwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (Wharfage) ambayo imeongezeka kutoka dola8.30  za Marekani  kwa ujazo wa tani moja hadi dola 10 za Marekani .

Kiasi hicho ni kwa ujazo wa tani moja, pamoja na ongezeko la Thamani (VAT).

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa ongezeko hilo  limelenga kuiwezesha (TPA) kuendeleza miradi mbalimbali inayohusu biashara ya mafuta, ikiwamo ujenzi wa gati mpya ya kupakua mafuta (SPM) na Ukarabati wa mifumo ya miundombinu ya Kurasini Oil Jetty (KOJ).

Ilitaja miradi mingine inayotekelezwa na TPA kuwa ni ujenzi wa maghala mapya na eneo la upokeaji mafuta (manifold)  na kwamba miradi itakapokamilika itaboresha kazi ya kupokea mafuta na pia itapunguza gharama za mafuta kumalizika kwa miradi hiyo.

Kutokana na bei hiyo mpya Petroli kwa jiji la Dar es Salaam itauzwa 1956,mafuta Dizeli Sh1977 na mafuta ya Taa Sh1963, Mwanza Petroli itauzwa  kwa Sh2106,Dizeli Sh2127 na mafuta ya taa Sh2112.

Katika jiji la  Arusha Petroli itauzwa  kwa bei ya Sh2040,Dizeli Sh2061 na mafuta ya taa Sh2047,Mbeya Petroli itauzwa  kwa Sh2063,Dizeli Sh2084 na mafuta ya Taa Sh2069.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA