BONDIA MOHAMMED ALI ATIMIZA MIAKA 70

Muhammad Ali atimiza miaka sabini


Ustadi, haiba na misimamo isiyoyumba ya Muhammad Ali ndio mambo yaliyosaidia kuufanya mchezo wa masumbwi kuwa maarufu duniani, kwa mujibu wa Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton.
Muhammad Ali atimiza umri wa miaka 70
Muhammad Ali atimiza umri wa miaka 70

"Alisaidia kuwafanya mamilioni ya watu kuamini. Alikuwa mtu wa pekee," alisema Clinton.
Bingwa mara tatu wa uzito wa juu Ali alishinda mapambano 56 katika muda wa miaka 21 wa kuzikinga ngumi ulingoni.
Pia aliweza kufanya mengi nje ya ulingo kwa maneno yake makali na kukataa kushiriki katika vita vya Vietnam.
Lakini Clinton anaamini Mmarekani mwenzake huyo ambaye alikuwa mtu maarufu sana duniani, umaarufu huo ulisaidia dunia nzima kuzungumzia mchezo wa masumbwi tena katika miaka ya 1960.
"Watu waliacha kuupenda mchezo wa ngumi. Katika miaka ya 1940 na 1950 ulikuwa ni mchezo maarufu sana Marekani na baadae umaarufu huo ukapotea," aliimwambia mtangazaji wa masumbwi wa BBC Mike Costello.
"Baadae akachomoza Muhammad Ali, awali akiitwa Cassius Clay, akionekana sawa na mcheza dansi katika ulingo wa masumbwi - akiwakumbusha watu huo ulikuwa ni mchezo.
"Aliurejeshea mchezo huo msisimko na kuwa wa maana tena. Alikuwa akiburudisha na alipokuwa kijana alikuwa akizungumza sana. Lakini ilikuwa ni sehemu ya madoido yake.
Ali alithubutu kuuweka hatarini mchezo na heshima yake, kwa kupinga vita vya Vietnma. Aligoma kujiunga na jeshi la Marekani wakati alipoitwa kulitumikia.
Mamlaka zinazosimamia mchezo wa masumbwi waliisimamisha leseni yake na kumvua mataji yake kabla ya kupatikana na hatia ya jinai baada ya kesi ya mwaka 1967. Mahakama Kuu ya Marekani ilitengua uamuzi huo miaka minne baadae.
Bingwa wa zamani wa masumbwi Uingereza na Jumuia ya Madola kwa uzito wa juu Joe Bugner aliyewahi kuzichapa na Ali mwaka 1973 na 1975, na kushindwa kwa pointi katika mapambano yote hayo, aliiambia BBC "ilikuwa ni heshima kubwa kupigana naye katika mapambano yote mawili."
"Alikuwa ni mwanamichezo zaidi ya mwanamasumbwi. Alikuwa ni mwanamichezo aliyekuwa na maarifa mengi, aliyekuwa akitumia kila inchi ya ulingo wa masumbwi."
Frank Bruno amesisitiza kamwe hataweza kumshuhudia bondia mwengine kama alivyokuwa Ali, ambaye anaamini aliiuweka mchezo wa masumbwi "katika ramani".
"Alifungua njia kwa wanamasumbwi kama mimi kupenda mchezo huo na kujipatia kipato," alisema Bruno.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA