Charles Taylor alikuwa jasusi wa CIA

Charles Taylor (kulia) anashtakiwa na mahakama ya ICC
Aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor alikuwa na uhusuiano rasmi na shirika la ujasusi la Marekani, CIA.
Mwandishi wa gazeti moja nchini marekani la Boston Globe, Bryan Bender, ameiambia BBC kwamba imemchukua miaka sita kupata jibu hilo kutoka kwa shirika hilo la CIA.
Kulingana na mwandishi huyo, Bwana Taylor alipotoroka kutoka jela moja mjini Boston Marekani mwaka wa 1985, aliishi nchini Libya, ambapo aliweza kutafuta habari kuhusu marehemu Kanali Gadaffi na kuwasilisha maelezo yake kwa shirika la ujasusi la Marekani la CIA.
Bwana Bender amesema serikali ya Marekani ilithibitisha kuwa uhusuiano kati yake na Bwana Taylor ulianza miaka ya themanini.
Mwandishi huyo ameiambia BBC kwamba shirika la ujasusi la idara ya ulinzi limesema kuna stakabadhi nyingi za siri zinazothibitisha uhusiano kati yao na Bwana Taylor.
Lakini shirika hilo halikutoa maelezo zaidi kuhusu yaliyomo katika stakabadhi hizo.
Bwana Bender anasema aliwasilisha ombi kwa shirika la ujasusi la idara ya ulinzi na pia shirika la CIA miaka 6 iliyopita, akitaka kuelezwa ikiwa Bwana Taylor alikuwa na uhusiano wowote na mashirika hayo.

Mahakama ya ICC

Wakati huo Bwana Taylor alikuwa akiishi uhamishoni nchini Nigeria na mahakama ya kimataifa ya jinai ya ICC ilikuwa imetoa kibali cha kukamatwa kwake.
Bwana Taylor alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita.
Bwana Bender anasema anadhani mojawapo ya sababu ya shirika hilo la ujasusi kutoa habari hizi mwishowe baada ya miaka sita huenda ikawa ni kwa sababu ya ukiritimba serikalini na pia kwa saabu huenda uhusiano huo ulikuwa umedumu kwa muda wa miaka thelathini.
Chini ya sheria za Marekani, maelezo fulani lazima yatolewe kwa umma baada ya miaka ishirini na tano.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA