GRACE MICHAEL AULA BUPAT


MWANDISHI wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael ameteuliwa
kuwa mjumbe wa Kamati ya Programu na Mafunzo ya
Chama cha Waandishi wa Habari za Bunge (BUPAT).
Uteuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya BUPAT
ambayo iliketi Dar es Salaam jana na kufikia uamuzi huo
ambao mbali na kuteua kamati hiyo pia iliteua na kamati
zingine mbili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BUPAT, na
kusainiwa na Oscar Mbuza, Kamati ya Programu na
Mafunzo itakuwa chini ya Uenyekiti wa Gabriel Zacharia
ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya BUPAT.
Katibu wa Kamati atakuwa Rodgers Luhwago na
wajumbe ni Joseph Lugendo, Grace Michael na
Deogratias Mushi.
Kikao cha uteuzi huo ambacho kilichokuwa chini ya
Mwenyekiti wa BUPAT, Godfrey Dilunga, Makamu
Mwenyekiti Gabriel Zakaria na Katibu Mkuu Leonard
Mwakalebela pia kiliteua Kamati ya Fedha na Uchumi na
Kamati ya Mawasiliano ya Umma.
Kamati ya Uchumi na Fedha, Mwenyekiti wa Kamati hiyo
atakuwa ni Charles Masyeba, ambaye pia ni Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya BUPAT. Katibu ni Bakar Mnkondo
na wajumbe ni Damas Kanyaboya, Agnes Tuniga na
Henry Mabumo.
Kamati ya Mawasiliano ya Umma itakuwa chini ya
Uenyekiti wa Oscar Mbuza, ambaye pia ni Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya BUPAT. Katibu ni Irene Mark na
wajumbe ni Chacha Maginga, Selemani Mpochi na Angelo
Moleka.
Taarifa hiyo, ilisema kuwa Kamati ya Utendaji ya BUPAT
imeamua kuwa Mweka Hazina wa BUPAT, Deborah Sanja
atakuwa mjumbe wa kamati zote kutokana na wadhifa
wake.
Kamati hizo zitafanya kazi zake kutokana na maelekezo
yatakayowasilishwa kwake na Kamati ya Utendaji ya
BUPAT.
Mbali na nafasi hiyo, Michael pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa habari wa Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA