Halmashuri zote hapa nchini
zinatarajia kutumia mfumo mmoja wa kihasibu ambapo kupitia mfumo huo taarifa za
kihasibu pamoja na takwimu mbalimbali za idara hiyo zitaweza kuonekana kwa
urahisi zaidi tofauti na mfumo uliokuwepo hapo zamani.
hayo yameelezwa leo na Bw
Jeremiah Mtawa ambaye ni Mwenzeshaji wa kitaifa wa mfumo huo kutoka Tamisemi
wakati akizungumza na waandshi wa habari mara baada ya kufungua mkutano kwa
wadau mbalimbali wa halmashauri mkoani hapa.
Bw Jeremiah alisena kuwa kwa
sasa mfumo huo utakuwa na faida kubwa sana hata kwa upande wa wahasibu ndani ya
halmashauri kwa kuwa mfumo huo ni raisi zaidi kiutendaji kuliko ule wa awali.
alibanisha kuwa pia mfumo
huo ambao unajulikana kwa jina la mfumo wa uhasibu usimamizi na udhibiti wa
fedha za umma utaweza kuraisisha shuguli mbalimbali za kihasibu.
"hapo awali mfumo wa
kihasibu uliokuwepo ulikuwa una mambo mengi sana lalkini kwa sasa mfumo huu
ambao unatumia teknolojia mbalimbali utaweza kusaidia sana kazi hii kwa msingi
wa hali ya juu sana"aliongeza Bw Jeremia.
pia alisema kuwa nao
watumiaji wa mfumo huo wanatakiwa kuwa makini sana na kuhakikisha kuwa wanafuta
taratibu na sheria mbalimbali za mfumo huo ili kufikia malengo mbalimbali ambayo
yamekusudiwa.
alianisha kuwa endapo kama
watafuata sheria na kanuni mbalimbali za mfumo huo basi halmashauri mbalimbali
hapa nchini zitaweza kuepukana na madhara mbalimbali huku kwa upande wa Serikali
nako malengo yake yakiweza kutimia . (kwa hisani ya Fullshangwe blog)
Comments