JK USO KWA USO NA DK SLAA WA CHADEMA

Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbrod . Slaa, wakati viongozi wa chama hicho walipofika Ikulu, Dar es Salaam kufanya mazungumzo na rais.

JK akisalimiana na Tundu Lissu

 JK akizungumza na viongozi wa CHADEMA Ikulu, Dar es Salaam
 JK akizungumza na Mwesiga Baregu wa CHADEMA alipokuwa akiwasindikiza baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa hicho hadi usiku wa saa 5:15
                        JK akiagana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe

RAIS Jakaya Kikwete amekutana na uongozi wa Chadema Ikulu Jijini Dar es Salaam, akiwemo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya.Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili, mkutano huo ulifanyika jana kuanzia saa 10:30 jioni na kuendelea hadi usiku, lakini walifanya mapumziko mafupi saa tatu usiku.

Ujumbe wa Chadema uliokuwa wa watu wanane, ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe. Wengine waliofuatana naye pamoja na Dk Slaa ni  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, John Mnyika, Said Arfi, John Mrema, Profesa Mwesiga Baregu na Profesa Abdallah Safari. Hadi tunakwenda mitamboni kikao hicho kilikuwa kinaendelea.


Hii ni mara ya kwanza kwa Dk Slaa kukutana na Rais Kikwete tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010, ambao Dk Slaa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 akiwa nyuma ya Rais Kikwete aliyepata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17, Dk Slaa hakuwahi kukutana na mkuu huyo wa nchi ana kwa ana.

Katika hafla ya kutangazwa matokeo ya urais iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, Dk Slaa hakuhudhuria tofauti na ilivyokuwa kwa waliokuwa wagombea wenzake wote.


Dk Slaa, ambaye alikataa kuyatambua matokeo hayo, tangu wakati huo hawakuwahi kukutana rasmi na Rais Kikwete huku uvumi ukizagaa kwamba  kwamba mwanasiasa huyo amekuwa akijaribu kukwepa asikutane ana kwa ana na Rais Kikwete kwenye mazingira yoyote.

Katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya chama hicho, Regia Mtema yaliyofanyika katika Kijiji cha Lipangalala, hivi karibuni Dk Slaa alidaiwa kumkwepa Rais Kikwete, kwa kutokwenda kukaa kwenye nafasi aliyoandaliwa jirani na kiongozi huyo mkuu wa nchi.


Ilidaiwa kuwa nyumba kulikofanyika shughuli za awali za mazishi, waandalizi waliandaa majukwaa mawili, moja maalumu kwa ajili ya wabunge huku jingine likiwa ni maalumu kwa ajili ya viongozi wakuu ambalo alikaa Mbowe, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe.

Mbali ya kukaa viongozi hao, kulikuwa na nafasi ambayo ilikuwa imetengwa maalumu kwa ajili ya Rais. Mbali ya nafasi hiyo, pia kulikuwa na kiti ambacho ilitegemewa kwamba Dk Slaa angekalia.

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo wa Chadema alidaiwa kukikwepa na kwenda kujichanganya katika jukwaa la wabunge na kiti hicho kubaki bila ya kukaliwa na mtu.

Hata hivyo Dk Slaa alikanusha uvumi huo na kudai kwamba asingeweza kwenda kukaa jukwaa alilokaa Rais Kikwete kwani yeye si kiongozi wa serikali hivyo kwa mujibu wa itifaki, asingeweza kumfuata Rais Kikwete na kwenda kumsalimia alipoketi.

Hii ni  mara ya pili kwa ujumbe wa Chadema kukutana na Rais Kikwete Ikulu  kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.