JONATHAN AMTIMUA MKUU WA POLISI NIGERIA

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amemfuta kazi kamishna wa polisi kutokana na ongezeko la visa vya mashambulizi yanayotekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram.

Taarifa kutoka ikulu ya Nigeria imesema kuwa Hafiz Ringim amelazimishwa kwenda likizo ya lazima huku akisubiri kustaafu rasmi.

Hatua ya kumstaafisha mapema mkuu wa Polisi , wiki chache tu kabla ya kustaafu rasmi inaonyesha jinisi gani swala la Boko Haram limeitatiza serikali ya Goodluck Jonathan.

Baada ya mashambulizi ya hivi karibuni ya kundi hilo la Boko Haram serikali imekuwa ikishinikizwa kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na hali hiyo.

Hivyo hatua ya kumtimua kazi mkuu wa polisi inaonekana kuwa ni njia mojawapo ya kuwafanya wa Nigeria wawe na imani na kikosi cha polisi cha nchi hiyo.

Ishara kuwa mkuu huyo wa polisi alikuwa amelemewa na kazi ni pale mshukiwa mkuu wa Boko Haram ambaye ana tuhumiwa kupanga mashambulizi katika kanisa moja na kusababisha vifo vya watu karibu 30 siku ya krismasi alipotoroka jela.

Mambo yalionekana kumlemea Hafiz Ringim, wakati alipotangaza kuwa atakabiliana vilivyo na kundi la Boko Harama hadi alimalize ,lakini siku chache baadaye kituo cha polisi kikashambuliwa na kundi hilo la Boko Haram.

Taarifa toka ikulu ya Nigeria inasema kuwa hivi karibuni kikosi kizima cha polisi kinatarajiwa kufanyiwa marekebisho ili kuimarisha utendaji kazi wake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*