KCB,SERENGETI, TANGACEMENT ZAJKABIDHI MSAADA KUADHIMISHA MIAKA 48 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ,Mama Asha Seif
Iddi akipokea msaada wa Madawati 144 kutoka kwa Meneja wa masoko wa
Benki ya KCB tawi la Zanzibar, Abdul Mshangama , madawati hayo kwa
ajili ya skuli ya Msingi ya Mwera yamekabidhiwa skulini hapo jana yana
thamani ya shilingi milioni 11.(Picha na Haroub Hussein).

MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ,Mama Asha Seif
Iddi akizungumza na wanafunzi wa skuli ya Mwera baada ya kupokea
msaada wa madawati 144 kutoka Benki ya KCB tawi la Zanzibar, kulia
Mwakilishi wa Jimbo la Koani Mussa Ali Hassan na Mbunge wa Jimbo hilo
Amina Andrew.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
akipokea msaada wa fulana kutoka kwa Mkurugenzi wa mahusiano na
mawasiliano wa Kampuni ya Serengeti Breweries LTD.Teddy Hollo Mapunda
, msaada huo umetolewa kupitia kinywaji chake  kisicho na kilevi cha
Malta Gunness una thamani ya shilingi milioni 15.unakwenda sambamba na
shamrashamra za kutimia miaka  48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
akipokea msaada wa fulana kutoka kwa Afisa mawasiliano wa kampuni ya
Saruji ya ‘Tanga Cement Ltd.’ kampuni hiyo ilitoa msaada wa fulana na
kofia zipatazo 2500 zenye thamani ya shilingi milioni 33.msaada ambao
unakwenda sambamba na Sherehe za kutimia miaka 48 ya Mapinduzi ya
Zanzibar,hafla iliyofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Vuga mjini Unguja jana.(Picha na Haroub Hussein).

 MKURUGENZI wa Mahusiano na mawasiliano wa Kampuni ya
Serengeti Breweries, Teddy Hollo Mapunda (katikati) akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani) muda mfupi baada ya kukabidhi
msaada wa fulana, wenye thamani ya shilingi milioni 15. kwa Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar , Balozi Seif Ali Iddi  kwa ajili ya Sherehe
za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.msaada huo ulikabidhiwa ofisini
kwa Makamu wa Pili wa Rais Vuga mjini Unguja jana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA