ZUKU TV WAZINDUA RASMI HUDUMA ZAO NCHINI

Mkurugenzi wa TCRA,Profesa John Mkoma akibonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya kuzindua Televisheni ya Zuku Africa kupitia kampuni ya Wananchi Satelite Tanzania inayotoa matangazo yake kwa kutumia ving'amuzi nchini Tanzania , Hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam jana jioni ikihudhuriwa na wadaum mbalimbali na wageni waalikwa. Katika picha kulia ni Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group na kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki wakishuhudia tukio hilo.
Mkurugenzi wa TCRA,Profesa John Mkoma mbele ya wageni waalikwa mbalimbali kabla ya kuzindua kampuni ya Wananchi Satelite jana katika hafla iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Golden Tulip kulia ni Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group na kulia ni Mwenyekiti wa makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki
Mwenyekiti wa makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki akizungumza katika uzinduzi huo na kumkaribisha Mkurugenzi wa TCRA Profesa John Mkoma. Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group akimkaribisha Mwenyekitiwa Makampuni ya Wananchi Group Ali Mufuruki.
Kundi la TMK wanaume Family likitumbuiza katika uzinduzi huo jana.
Bendi ya Tanzanite ikiongozwa na mwanamzuiki nguli John Mhina ilitoa burudani ya kutosha katika uzinduzi huo jana.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika uzinduzi huo.
Wadau hawa nao walikuwepo ndani ya nyumba kama unavyowaona wengi wanaipenda ZUKU TV.
Waimbaji wa muziki wa injili pamoja na waigizaji wa filamu hawakukosa uzinduzi huop kutoka kulia ni Mwigizaji Natasha, Monalisa , Mwimbaji Alice na mumewe ambaye pia ni mwimbaji Bw. Robert David wakipozi kwa picha.
Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group katikati na Mwenyekiti wa makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki kulia wakimsikiliza Meneja mkuu wa Wananchi Satelite Bw Mohamed Jeneby akiwaelezea jambo.
Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group kulia i na Mwenyekiti wa makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki wakijadili jambo katika uzinduzi huo.
Wadau kutoka ZUKU TV wakipozi kwa picha jana katika uzinduzi huo.
Mwanamuziki AY na wenzake walihudhuria pia uzinduzi huo.
Jaquiline Karanja kulia na Moureen walikuwepo pia hebu wacheki na pozi yao.
Mamaa Shamimu Mwasha a.k.a. ZEZE wa http://8020fashions.blogspot.com/akitafuta taswira katika uzinduzi huo, kuminya jicho ni lazima kama unataka taswira iliyotukuka.
Kutoka kulia ni wadau ZIZZOU wa ZIZZOU Fashion, Suzy wa Clouds na mdau Godliver wa Prime Time wakipozi kwa picha. (PICHA KWA HISANI YA BLOG YA FULLSHANGWE)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA