MAADHIMISHO MIAKA 48 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

DK. SHEIN: TUTAENDELEA KUYALINDA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk Shein wakifurahia jambo
wakati wa sherehe hizo leo
Na Antar Sangali, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesisitiza msimamo wake wa kuendelea kuyalinda, kuyasimamia na kuyaendeleza kwa hekima malengo ya Mapinduzi ya Janua12, 1964.


Rasi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhamed Shein ametoa msimamo huo katika kilele cha maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizoadhimishwa katika uwanja wa Amani mjini Unguja.


Dk Shein amesema Serikali yake itaendelea na mikakati wa kuboresha maisha ya wananchi, kuwapatia elimu bora, kuinua hali za wakulima wavuvi, na wafugaji bila ya ubaguzi au upendeleo.


Amesema pamoja na dhamira ya kuleta neema kwa wananchi wote ni lazima jamii ikatambua  umuhimu wa kulinda na kuiendeleza msingi ya iliyojenga amani, umoja,utulivu  na mshikamano wa kitaifa.


Hata hivyo mhe Rais wa Zanzibar amewaeleza wananchi na kuwahakikishia kuwa mpango wa Serikali yake wa kusambaza maji safi na salama, kujenga vituo vya afya,ujenzi wa shule  na barabara, vitafanyika kwa umakini na mazingatio ya kisera.


Rais huyo wa Zanzibar awamu ya saba amewaambia bayana wananchi kuwa Serikali yake itaendelea kuwa shirikishi huku ikiweka mkazo zaidi katika mapambano dhidi ya maadui ujinga umasikini na maradhi.

Aidha Dk Shein amesifu utulivu,mazikizano na maelewano yanayoendelea kuimarika miongoni mwa wananchi na viongozi wa Serikali huku akisema hilo ni jambo la faraja kwa maendeleo ya Zanzibar mpya.


Dira na malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 1964 yalikusudia kurejesha thamani ya utu wa watu wanyonge , heshima na hadhi ya kila wananchi aliyebaguliwa na kunyimwa haki za kibinadamu.


Katika maadhimisho ya sherehe hizo viongozi kadhaa wa kitaifa wamehudhuiria akiwemo Rais wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete, Makamo wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal  ,Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda , Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange na IGP Said Mwema .

Wenginme ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd na marais wa wastaafu wa awamu ya Pili na Tatu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi na  Mzee Benjamin William Mkapa.


Viongozi wengine ni Waziri Mkuu mstaafu Feredrick Sumaye, Edward Ngoyai  Lowassa,Waziri Kiongozi mstaafu wa wamu ya pili Ramadhan Haji Faki, Wazir Kiongozi mstaafu awamu ya sita Shamsi Vuai Nahodha, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania na wananchi mbalimbali.


Vikosi vya ulinzi na Usalama vilipita kwa heshima mbele ya Rais Dk Ali Mohamed Shein kutoa heshima zao, vijana wa halaiki wapatao 500 wakaonyesha michezo ya ushupavu na ukakamavu huku mizinga 21 ikipigwa kwa heshima.


Maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi  ya Zanzibar ni matokeo ya kufuzu mpango makakati wa chama cha ASP kuupindua utawala wa Sultan na alia yake uliodumu kwa zaidi ya karne mbili Visiwani humu.


HABARI KATIKA PICHA
 Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akikagua garide wakati wa sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aaman mjini Unguja.
 Rais Wanzibar Dk Shein akimsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete, Wengine waliopo pichani kwa karibu karibu ni makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasasa
 Rais Mstaafu Benjamin \mkapa akimsalimia Rais Dk. Sheni
 Rais Kikwete akimsailimia Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad


Rais Kikwete na Rais Dk. Shein  wakiwa na v Viongozi wakiwa kwenye sherehe hizo
 Maalim Seif, Mama Salma Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa kwenye sherehe hizo
 Moshi wa mizinga iliyopigwa ukitanda baada ya kulipuliwa kusherehesha sherehe hizo
Msafara wa rais wa zanzibar ulkiingia mwanzoni mwa sherehe hizo (PICHA ZOTE NA IKULU)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA