MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 35 YA CCM MWANZA

Vijana wanaoshiriki mazoezi kwa ajili ya gwaride maalum la sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM wakipumzika baada ya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Vijana wanaofanya mazoezi ya gwaride maalum wakitoka kwenye Uwanja wakati wa mapumziko baada ya mazoezi hayo leo.

Vijana hao wanaoshiriki mazoezi ya gwaride maalum la miaka 35 ya CCM, tangu waweke kambi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, hupata mahitaji yao hapo ikiwemo chakula. Pichani chakula kikiandaaliwa kwenye Uwanja huo

Vijana wa kike wakionyesha ukakamavu wao wakati wa mazoezi ya gwaride maalum la umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM zitakazofanyika Kitaifa jijini Mwanza.

Vijana wakiwa katika mazoezi ya kutembea kwa ukakamavu, wakati ma mazoezi ya maandalizi ya gwaride maalum la vijana wa CCM kwa ajili ya kilele cha miaka 35 ya CCM, leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Viongozi wa gwaride hilo wakiwa mazoezini leo kwenye wanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza zitakakofanyika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM.

Vijana kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza wamo katika mazoezi ya gwaride maalum kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM yatakayofanyika Kitaifa mkoani humo, Februari 5, mwaka huu. Pichani, baadhi ya vijana hao wakiwa katika mazoezi ya gwaride kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Brass band itakayoongoza gwaride maalum la Vijana wa CCM, ikiwa katika mazoezi leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA