Majambazi Yapanga Mawe Na Kupora Manyoni..






Ndugu zangu,

Niliondoka Singida Mjini saa kumi na moja alfajiri kuelekea Dodoma. Kilomita 40 kutoka Manyoni nilikutana na hali hiyo pichani kunako saa kumi na mbili na nusu. Eneo la tukio niliwakuta askari watano wamevalia kiraia wakiwa na silaha za moto. Wameniambia tukio limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya kuanzia saa sita usiku na linawahusisha maja majambazi wasiopungua wanane.

Kuna walioporwa fedha, simu na mali zao . Mahali hapa kuna pori kubwa upande wa kushoto. Inaaminika majambazi hayo yenye silaha yangali yamejiicha porini.
Hakuna aliyekamatwa. Nilishuhudia polisi hao wakifuatilia nyayo huku wakinionyesha mahali majambazi hayo yalilala chini kujificha wakisubiri giza na kuanza kupanga mawe yao. Kwa kusoma mazingira ya eneo kwangu mimi napata tafsiri kuwa majambazi hayo yalifanya maandzi ya mpango wao kwa siku kadhaa.

Maana, mawe hayo mazito yanaonekana kuwa yalikuwa yakisogezwa usiku karibu na tukio na kufikia idadi waliyohitaji. Intelijensia ya kipolisi ingefanya kazi yake sawa sawa na kwa kushirikiana na wenyeji ingewezeza kubaini mapema movement ya mawe yale. Na katika dunia ya sasa , mbwa wa polisi waliopewa mafunzo wangefanya kwa haraka na kwa ufanisi zoezi la kufuatilia majambazi porini badala ya polisi kufuatilia nyayo kwa macho.
Maggid Mjengwa,
Dodoma, Januari 27, 2012

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA