Mkufunzi Josef Diouf kutoka Shirikisho la masumbwi Dunia (AIBA) atua nchini

Na Mwandishi wetu SHIRIKISHO la Ngumi za ridhaa nchini (BFT) limepiga panga baadhi ya majina ya makocha walioteuliwa kushiriki katika kozi ya kimataifa ya mchezo huo iliyopangwa kufannyika kesho Januari 16 mwaka huu. BFT imewakata washiriki hao baada ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki kutokana na hasara iliyosababishwa na washiriki hao katika kozi ya awali iliyokuwa ifanyike tangu mwezi Novemba mwaka jana. TOC ambayo huandaa kozi za michezo mbalimbali kutokana na ruzuku inayotolewa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) ilikuwa iendeshe kozi hiyo tangu mwaka jana lakini haikufanyika kutokana na mkufunzi wa kozi hiyo kutoka nchini Algeria kuingia mitini, Kozi hiyo ya Kimataifa ya Mchezo wa masumbwi kwa mara ya mwisho ilifanyika nchini mwa 2002 ambapo ni ngazi ya juu kabisa ya ukocha Duniani kote
TOC ililazimika kuwalipa nauli baadhi ya washiriki waliotoka nje ya Dar es Salaa kutoka katika fungu la pesa za kuendeshea kozi hiyo hivyo kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki hasa wale waliofanya utovu wa nidhamu katika kozi ya awali ili kiwango cha pesa kilichobaki kutosheleza mahitaji wa kozi itakayoendeshwa Januari 16 mwaka huu. Akizungumza Dar es Salaam Katibu mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema idadi ya makocha 25 waliowateua inaweza ikapungua tena kulingana na bajeti waliyobaki nayo TOC ambapo hata hivyo hakuyataja majina matano ya washiriki walioachwa . Aliwataja washiriki waliopenya kuhudhuria kozi hiyo ni mpiga picha wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na Jarida la Maisha ambaye pia alikuwa bondia, Rajabu Mhamila 'Super D', Anord Ngumbi, Moses Lema, Anthon Mwang'onda na Edward Emanuel (Dar es Salaam). Wengine ni Yahaya Mvuvi (Tabora), Joseph Mayanga na Zakaria Mwaseba (Morogoro), Omari Saady na Mussa Bakari (Mwanza), Ally Ndee (JKT Mbeya), Emilio Moyo na Gaudens Uyaga (Pwani) Juma Liso (Magereza Kigoma), Lyinda Kalinga (Dodoma) na Abdalah Bakari (Tanga). Wengine ni Mohamed Hashim (Polisi Dar es Salaam), David Yombayomba, Haji Abdalah, Said Omari (JWTZ), Mazimbo Ally, Rogated Damian na Fatuma Milanzi (JKT), Musa Maisori na Hamisi Shaaban (Magereza Dar es Salaam). Kozi hiyo itaendeshwa na mkufunzi wa kimataifa Josef Diouf kutoka Shirikisho la Dunia la mchezo huo (AIBA) ambaye atashirikiana na makamu wa Rais wa BFT, Michael Changarawe. Kozi hiyo itafanyika katika shule ya Sekondari ya Filbert Bayi Kibaha Mkoani Pwani na itafikia tamati Januari 24 mwaka huu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA