MKUU WA MKOA RUKWA ATEMBELEA MKANDARASI AASLEFF BAM INTERNATIONAL ANAYEJENGA BARABARA YA LAELA-SUMBAWANGA , ATANGAZA VITA NA WEZI WA MAFUTA NA VIFAA
Eneo
hili ambalo lipo nje kidogo na kambi ya Mkandarasi huyo linatumika kwa
ajili ya uchimbaji, upasuaji, na hatimaye utengenezaji wa kokoto kwa
ajili ya kuweka lami katika barabara anayojenga mkandarasi huyo.
Aasleff Bam International inajenga barabara ya Laela- Sumbawanga (95.31
Km) kwa kiwango cha lami. Barabara ya Tunduma- Laela- Sumbawanga
kufikia kiwango cha lami imegawanywa sehem kuu tatu ikiwemo Tunduma-
Ikana (63.7 Km), Ikana- Laela (64.2 Km ) na Laela- Sumbawanga (95.31 Km
).
Kwa habari na picha zaidi Tembelea hapa:http:http//:www.rukwareview.blogspot.com/
Barabara
hii inaendelea kujengwa na mpaka sasa kipande hiki cha Laela-
Sumbawanga kinachojengwa na Aasleff Bam Internatinal kimeshakamilika
kwa takriban aslimia 25% na tayari kuna kilomita 10 za majaribio
zimeshawekwa lami. Kandarasi huyo pamoja na wengine waliopo Mkoani
Rukwa wanatakiwa kukabidhi barabara zote mwanzoni mwa mwaka 2013.
Kutoka
muda uliopangwa Mkandarasi huyu ameomba kuongezewa muda wa miezi minne
kutokana na sababu kuu tatu, moja ikiwa ni kuchelewa kufika kwa vifaa
vya ujenzi walivyoagiza kutoka nje ya nchi, kucheleweshwa vifaa hivyo
bandarini kwani vilichukua muda wa miezi minne, na ukubwa wa kazi
iliyopo kuwa chini ya makisio yao hivyo kuchukua muda mwingi wa
majadiliano namna ya kukamilisha kazi kubwa kwa gharama za makisio
madogo.
Injinia
Manyanya akishikana mikono na mmoja wa makandarasi wa Aasleff Bam mara
baada ya kupewa maelezo juu ya mashine inayoonekana nyuma yao ya
kuchanganya udongo na cement. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga
Kanali John Antonyo Mzurikwao na Kushoto ni Meneja wa Tanroads Mkoa wa
Rukwa Kabaka Florian Mwombeki.
Msafara wa Mkuu wa Mkoa ukipokea maelezo kutoka kwa Mkandarasi wa Aasleff Bam kuhusu ujenzi wa barabara unaoendelea.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wakandarasi wa
Kampuni ya Aasleff Bam International ya Uholanzi inayojenga barabara
ya Laela - Sumbawanga kwa kiwango cha lami katika Mkoa huo. Mkuu huyo wa
Mkoa alilazimika kufanya ziara kujionea hali ya ujenzi inavyoendelea
pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa Kampuni hiyo. Kulia ni Mashine
aina ya mixer inayochanganya udongo na cement na kunyoosha barabara
kabla ya kokoto ngumu na lami kuwekwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wazawa wa
kampuni ya Aasleff Bam International ya Uholanzi inayojenga barabara ya
Laela - Sumbawanga kwa kiwango cha lami. Aliomba kuzungumza na
wafanyakazi hao kutokana na kulaumiwa kuiibia kampuni hiyo vifaa
ikiwepo mafuta ya diesel zaidi ya lita 30,000, tani 40 za simenti , na
nondo zaidi ya tani 300.
Mkuu
huyo wa Mkoa aliwaasa wafanyakazi hao kuwa na moyo wa kizalendo kwa
kuona kuwa kazi anayofanya kandarasi huyo italeta manufaa kwao.
Alitangaza vita na yeyote yule atakayethibitika kuhusika na wizi katika
kampuni hiyo pamoja na kampuni zingine zinazofanya kazi hiyo ya ujenzi
Mkoani Rukwa. Alisema kuwa ni aibu kuona wizi wa namna hiyo kwani kazi
anayofanya kandarasi huyo ni kwa manufaa ya watanzania wenyewe.
Comments