MOHAMMED DEWJI APOKEA MSAADA WA BAISKELI ZA WALEMAVU.


Pichani Juu na Chini ni Mh. Mohammed Dewji akipokea msaada wa Baiskeli Tano za Walemavu kutoka kwa Mkuu wa Club za wanachama wa Lions Club Tanzania na Uganda Satish Sharma.

Na.Mwandishi wetu.

Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Dewji amepokea msaada wa baiskeli 5 za walemavu kwa ajili ya jimbo lake zilizotolewa na Taasisi ya Lions Club Tanzania.

Mh. Dewji amekabidhiwa msaada huo leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Club za wanachama wa Lions Club Tanzania na Uganda Satish Sharma, katika makabidhiano yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Gerezani.

Mh. Dewji ameshukuru msaada huo akisema utakua faraja kwa wananchi wa jimbo lake ambao wanamatatizo ya ulemavu wa viungo.

“Nawashukuru Lions Club kwa msaada huu na utakua chachu kwa wananchi wa jimbo la Singida hususani walemavu wakiwemo wale wa viungo walio na mahitaji maalum, kwa kuwa baiskeli hizi zitawasaidia sana hivyo nawashukuru” amesema Mh. Dewji.

Kwa upande wake Satish Sharma amesema licha ya kukabidhi msaada huo wa baiskeli za walemavu, Lions Club wametoa misaada mbalimbali kwa nchi za Tanzania na Uganda, ikiwemo baiskeli hizo na vifaa mbalimbali vya shule.

“Kwa sasa Lions Club tunaendelea kutoa misaada mbalimbali ya kijamii vikiwemo vifaa vya mashuleni na michango mingine ikiwemo baiskeli na baada ya hapa tutaazunguka mikoa ya Morogoro na kisha kanda ya Ziwa mikoa ya Mwanza, Msoma, Bunda na Shinyanga” amesema Satish.

Lions Club mpaka sasa ina wanachama 1600 na Club 48 kwa nchi za Tanzania na Uganda, ambapo wamekua mstari wa mbele katika kusaidia misaada ya kijamii kwa nchi mbalimbali zilizo na wanachama Duniani kote.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA