MSD YATOA MSAADA WA SH.MIL.10 KWA TWIGA STARS

Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah hundi yenye thamani ya sh. mil. 10 ikiwa ni msaada kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga Stars, katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia. Timu hiyo inapambana na Namibia kesho katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake.
Katibu Mkuu TFF, Angetile Osiah (kushoto) akitoa shukurani kwa MSD kuipatia timu hiyo msaada. Kutoka kulia ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael na Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo
Katibu Mkuu TFF, Angetile Osiah (kushoto) akitoa shukurani kwa MSD kuipatia timu hiyo msaada. Kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo

Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo (kushoto) na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah wakiwa na furaha wakati wa hafla ya MSD, kukabidhi msaada wa Sh. Mil. 10 kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga Stars, Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia.
Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia (kushoto), akielezea umuhimu wa msaada huo kwa timu hiyo ya soka kwa wanawake. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah.

Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuhakikisha kiwango cha michezo kwa wanawake kinakuzwa, Bohari ya Dawa (MSD) imeiunga mkono Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga stars) kwa kutoa sh. milioni 10 ili ziweze kuisaidia timu hiyo.

Akikabidhi hundi hiyo Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki, Lucy Nderimo, alisema kuwa Bohari hiyo imefikia hatua hiyo ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vyema na hatimaye kuleta sifa kwa Tanzania.

"Leo timu yetu itakuwa kwenye mchuano na Namibia hivyo tumeona nasi tuwange mkono kwa hiki kidogo tulichonacho, kama mnavyofahamu michezo ni afya na sisi ni wadau wakubwa wa sekta hii," alisema Nderimo.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osia ambaye ndiye alipokea hundi hiyo, aliipongeza MSD kwa uamuzi wake huo ambao utatoa chachu kwa timu hiyo kuweza kufanya vizuri ikiamini kuwa inaungwa mkono na wadau wengi.

"Kwanza niseme tu niwashukuru kwa dhati kabisa, kwani hata tulipoamua kuandika barua kwa wadau mbalimbali hatukuwahi kuwafikiria nyie kama MSD, lakini kwa kitendo mlichokifanyainaonesha wazi namna mnavyoshirikiana na jamii katika nyanja zote na kupitia michezo tunaweza kushirikiana kuielimisha zaidi jamii kuhusu hata mambo mbalimbali mnayoyafanya," alisema Osia.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka wadau wengine kuziunga mkono timu za Taifa ikiwemo hiyo ya wanawake ili hatimaye ziweze kufikia kiwango kinachotakiwa na kuleta sifa kwa nchi.

Naye Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano, Salome Mallamia alisema kuwa timu ya wanawake imesahaulika hasa katika kuwanga mkono hali ambayo imeusukuma uongozi wa MSD ili kuhakikisha wanawake wanainuliwa na kuwezeshwa katika kufikia mafanikio.

"Huu ni mwanzo wa MSD kuchangia kundi la wanawake ambalo lilisahaulika lakini nia yetu ni kuhakikisha tunawaunga mkono kwa hali na mali na tutashirikiana na TFF kuhakikisha michezo inaendelezwa bila kujali timu ya wanawake au wanaume," alisema Mallamia.
Cioooo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA