MWANRI AWASHAMBULIA WANAOPINGA UTENDAJI WA SERIKALI YA JK


Na Francis Godwin,Mufindi

NAIBU waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Agrrey Mwanri amewataka wananchi kuwapuuza viongozi wa vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakihamasisha wananchi kuichukia serikali ya Rais Jakaya Kikwete bila kuwahamasisha vijana kufanya kazi kwa kujituma.

Alisema kuwa kila kukicha kumekuwa na migomo na maandamano ya kudai haki zao bila viongozi hao kuwahamasisha vijana hao kufanya kazi badala ya kuendelea kukaa vijiweni na kufanya maandamano ya kudai maisha bora bila kufanya kazi.

Akiwaahutubia wakazi wa Lugorofu Mgololo wilaya ya Mufindi Jana Mwanri alisema kuwa vijana wasikubali kutumikishwa na vyama hivyo vya siasa ambavyo sera zake ni kuikosoa serikali iwe kwa jema ama bay a na mud a wote wao ni kufanya maandamano ya kuipinga serikali.

Hivyo aliwataka vijana kufanya kazi kwa nguvu zote na Kuacha kuendelea kushinda vijiweni na kulalamikia ugumu wa maisha.

Katika hatua nyingine Mwanri amepiga marufuku Halmashauri kuendelea kutoa kazi kwa wakandarasi ambao wamekuwa wakija na vibarua wao katika kutekeleza miradi ya ujenzi katika Halmashauri husika na kuwa ni vema wakandarasi hao kuwatumia wananchi na vijana wa eneo husika na sio nje ya mradi .

Naibu waziri huyo Mwanri kwa Mara ya kwanza amepongeza kazi nzuri ya ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji Mgololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa mradi uliojengwa kwa kiasi cha zaidi ya shillingi bilioni moja na kuagiza maofisi ugani katika Halmashauri hiyo na Halmashauri nyingine za mkoa wa Iringa kutoka maofisini na Kwenda mashambani kusaidia

Katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi jana ,Mwanri alisema kuwa Amevutiwa na kazi nzuri ya usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo ya Mufindi na kuwa baadhi ya Halmashauri za mkoa wa Iringa wakurugenzi wake na wahandisi wa miradi ya ujenzi na maji Kama wilaya ya Ludewa wameshindwa Kabisa kuwajibika katika kusimamia fedha za serikali na wahisani katika miradi hiyo.

Hivyo alisema kuwa Wizara yake haitawafumbia macho watendaji wabovu wanaoshindwa kusimamia miradi hiyo ya maendeleo na kuwa katika ziara yake Halmashauri ya wilaya ya Mufindi imeonyesha kuwa ni Halmashauri ya mfano kwa kuwa na mradi mzuri wa umwagiliaji ambao bado kukamilika ila ni mradi wenye Sita zote za kuitwa mradi wa umwagiliaji.

Mwanri alisema kuwa pamoja na kuwa mradi huo bado kukamilika ila amelazimika kuruhusu uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi kupitia mkurugenzi wake Shimwela Limbakisye na mhandisi wa mradi huo Awariywa Nnko kuwaruhusu wananchi kuanza kuutumia mradi huo wakati jitihada za kuukamilisha zikiendelea

"Ndugu zingu viongozi wa wilaya ya Mufindi na mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarita Kalalu naomba kuwapongeza
San a kwa kazi nzuri mliyoifanya katika kusimamia miradi ya maendeleo katika Halmashauri yenu ....naomba kazi hii mzidi kuifanya kwa nguvu Kama hizi ili kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi zaidi"

Katika hatua nyingine Mwanri aliwataka wananchi wa Mgololo na wakazi wa wilaya ya Mufindi kuendelea kuutumia miradi hiyo kwa kuboresha maisha yao na kuwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeendelea kuboresha maisha ya watanzania kwa kuanzisha kusogeza maendeleo mbali mbali kwa wananchi wake.

Alisema kuwa wapo baadhi ya watu ambao wanaendelea kupinga kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Rais Kikwete na kuwa wananchi wasikubali kudanganywa na wapinga maendeleo hao Kwani hawataki kuona serikali ikiwasaidia wananchi wake ili wapate kuichafua serikali.

Akizungumzia maofisi agani katika Halmashauri ambao wamekuwa wakishinda maofisini walipata kiyoyozi na kuvaa suti badala ya Kwenda mashambani kwa wakulima kuwasaidia kujua na kulima kwa kuzingatia taratibu bora za kilimo.

Hivyo aliagiza kuanzia sasa Maofisa hao wanaowajibika kwa wakulima na wafugaji kutoka ofisini na Kwenda kuwajibika kwa wakulima na wafugaji katika vijiji badala ya kushinda mijini na ofisini wakishindana kuvaa suti.

Kwa upande wake mhandisi mradi wa umwagiliaji katika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Bw.Nnko alimweleza naibu waziri huyo kuwa mradi huo wa umwagiliaji Mgololo una zaidi ya heat 1,000 ambazo zitanufaisha kay a 1,808 zanye wakazi 7,693.

Alisema kuwa kazi ya ujenzi wa mfereji huo wa umwagiliaji inafanywa na mkandarasi Boimanda Modern construction co.Ltd ya mkoani Iringa chino ya mkurugenzi wake Nicholaus Mgaya na kuwa kiasi cha zaidi ya shillingi bilioni 1.4 zitatumika kukamilisha mradi huo.

Nnko alisema kuwa baada ya mradi huo kukamilika hekta 700 zitalimwa na kumwangiliwa hivyo kufanya wananchi zaidi ya 7693 wa vijiji vya Lugorofu na Makungu kufaidika na mradi huo na kuwa mazao yatakayolimwa katika mradi huo ni mpunga ,Mahindi ,maharage na bustani za mboga mboga.

Wakati huo huo Mwanri ameagiza wananchi na Halmashauri za wilaya nchini kusaidia kujenga vituo vya polisi katika vijiji na kata ili kusaidia kupambana na wimbi la uharifu katika maeneo ya vijijini.

Alisema kuwa uharifu umekuwa ukiendelea kutokuwa maeneo ya vijijini kutokana na serikali kusahau kujenga vituo vya polisi katika maeneo ya kata na hivyo kutaka wananchi na Halmashauri kushirikiana kujenga vituo vya polisi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA