NAIBU JAJI MKUU WA KENYA ASIMAMISHWA KAZI

Rais Mwai Kibaki amemsimamisha kazi Naibu Jaji Mkuu Nancy Baraza na kuunda jopo ambalo litafanyia uchunguzi mwenendo wake kutokana na shutuma zinazomkabili.

Jaji Baraza, anashutumiwa kumtishia maisha kwa bastola mlinzi wa duka moja kubwa, Bi Rebecca Kerubo wakati wa mkesha wa mwaka mpya.

Jopo hilo litaongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhan kama Mwenyekiti.

Wajumbe wengine ni Prof Judith Behemuka, Philip Ransley, Surinder Kapila, Beuttah Siganga, Grace Madoka na Prof Mugambi Kanyua.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ikulu ya Nairobi, Rais Kibaki alisema wakati wa uchunguzi,Bi Baraza hatoendelea na majukumu yake ya idara ya mahakama.

" Kwa wakati huu, Mheshimiwa Jaji Nancy Makokha Baraza, Naibu Jaji Mkuu, Mahakama ya juu ya Kenya amesimamishwa kazi mara moja kwa mujibu wa kifungu 168(5) cha katiba." Alisema rais Kibaki.

Katika muda huo atakaokuwa amesimamishwa kazi, Jaji Baraza, atakuwa anapata nusu mshahara hadi pale uchunguzi utakapokamilika na kufahamika kupitia mapendekezo ya jopo kama atarejeshwa kazini au atimuliwe.

Kuundwa kwa jopo kumetokana na mapendekezo yaliyowasilishwa kwa rais Kibaki na tume inayoshughulika na masuala ya idara ya mahakama iliopendekeza Baraza asimamishwe kazi na uchunguzi juu ya mwenendo wake ufanywe.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA