NAPE KUUNGURUMA STAR TV KESHO ASUBUHI, KUHUSU MAADHIMISHO YA MIAKA 35 YA CCM

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnaune kesho atakuwa katika studio za Kituo cha Televisheni cha Star Tv jijini Dar es Salaam, kuzungumzia kwa kina 'mpango mzima' wa maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM, yatakayofikia kilele Februari 2, 2012.

Wakati Nape (Pichani) atakuwa katika studio za jijini Dar es Salaam, katika kipindi hicho kitakachorushwa kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7.30 am), Kada wa CCM Frank Uhahula atakuwa akizungumzia suala hilo hilo akiwa katika studio namba moja za Star Tv zilizopo jijini Mwanza.

Bila shaka hii itakuwa fursa nzuri kwa wale wote wenye dukuduku la kutaka kufahamu kwa kina mambo mengi kuhusiana na maadhimisho hayo ya miaka 35 ya CCM 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, Mapema mwezi huu kuhusu maadhimhso hayo, Nape alisema katika maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM mambo mengi yatajiri.
Nape alisema kwa kuwa maadhimisho hayo yanafanyika wakati uchaguzi mkuu wa chama unakaribia, Chama kitayatumia kupiga vita wagombea wote wanaotoa na kupokea rushwa wakati wa uchaguzi huo.

Pia kitatumia maadhimisho hayo kuhamasisha wananchama wake waadilifu na waaminifu kujitokeza kugombea katika uchaguzi huo utakaofanyika mwaka huu, kuanzia ngazi za mashina hadi taifa.

Nape alisema, Chama kitatumia fursa hiyo pia kuwaelimisha wanachama wake na wananchi kwa jumla kuhusu mabadiliko ya Katiba ya nchi yanayokusudiwa kufanyika, ikiwa ni pamoja na msimamo wa kuilinda nchi, amani, na kupatikana kwa Katiba bora itakayokuwa na manufaa kwa watu wote.

Alisema, maadhimisho hayo yataanza Januari 30, mwaka huu kwa shughuli mbalimbali zilizoratibiwa katika ngazi mbalimbali za Chama mikoani hadi  Februari 5, 2012 maadhimisho hayo yatakapohitishwa kwa matembezi ya mshikamanoo yatakayofanyika kila mkoa wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo kitakachofanyika kitaifa mkoani Mwanza.

"Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu kwa Chama Cha Mapinduzi kufikisha miaka 35 ya uhai wake yangu vyama vya TANU na ASP vilipovunjwa na kuundwa chama kipya cha CCM chenye nguvu, Februari 5, 1977",lisema Nape na kuongeza.

"Sherehe hizo huadhimishwa kwa Chama na Jumuia zake kufanya shughuli mbalimbali za kisiasa na kijamii. Aidha, Kitaifa Chama huteua mkoa mwenyeji wa sherehe hizi ambazo huambatana na matembezi ya mshikamano".

Alisema kwa kuwa mwaka huu ni wa Uchaguzi Mkuu wa Chama kimependekeza kaulimbiu mahsusi itakayotumika katika sherehe hizo kuwa ni "CCM Imara na Madhubuti inaanza na mimi; naimarisha Chama Changu kwa kuchagua viongozi bora na waadilifu".

Nape alisema uzinduzi wa sherehe hizo utafanyika kila mkoa Januari 30, mwaka huu na kufuatiwa na wiki ya shughuli za Jumuia, ambazo kila Jumuia itapanga ratiba ya mikutano ya ndani na shughuli za kijamii kama kupanda miti, ukaratabti wa shule, zahanati na kadhalika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA