NDOTO YA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI YATIMIA,

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kushoto), akibadilishana hati za makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ujenzi ya  China Railway Engineering Group Co. Limited, Shi Yuan baada ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Dar es Salaam . Wanaoshuhudia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick (katikati) na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

Dk. Dau akitiliana saini na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni itakayojenga daraja la Kigamboni, Dar es Salaam, Shi Yuan

Wakibadilishana hati za mkataba huo

Waziri wa Kazi na Ajira, Kabaka akihutubia wakati wa hafla hiyo

Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Abubakar Rajab, akitoa shukrani kwa Serikali

Wakiwa katika picha ya pamoja baada kusaini mktaba

 Dk. Dau akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salalaa, Said Sadick
 Waziri wa Ujenzi akijadiliana jambo na Mtangazaji wa Radio Clouds, Ephraem Kibonde aliyekuwa MC wa hafla hiyo
                                     Magufuli akiwa katika picha ya moja na baadhi ya wapigapicha za habari
Na Richard Mwaikenda

UJENZI wa daraja jipya la Kigamboni, utakaogharimu sh. bilioni 214 unatarajia kuanza mwezi ujao baada ya kutiwa saini mkataba jijini Dar es Salaam leo.

Mkataba huo, ulitiwa saini na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ujenzi ya China Railway Construction Engineering Group Co Ltd, Shi Yuan.

Utiaji saini mkataba ulishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick na baadhi ya viongozi kutoka wizara hizo. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, hakuhudhuria kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kitaifa.

Mkurugenzi  Mkuu wa NSSF, Dk Dau alisema kuwa katika mradi huo, NSSF itatoa asilimia 60 ya gharama  na Serikali itatoa asilimia 40.

Alisema mradi huo, utahusisha maeneo makubwa yafuatayo; Ujenzi wa njia sita (6) za lami umbali wa km 1.0 kwa upande wa Kurasini, ujenzi wa mita 680 za daraja (Cable stayed Bridge) na  ujenzi wa njia sita (6) za lami umbali wa Km 1.5 kwa upande wa Kigamboni.

Alisema ndoto ya ujenzi wa daraja la Kigamboni ulianza mwaka 1977, lakini utekelezaji haukuwekana kwa sababu ya ukosefu wa fedha, ambapo wakati huo ungegharimu Dola za Kimarekani 33,400,000.

Mwaka 1991, ulifanyika upembuzi yakinifu mwingine wa mradi huo, na kuonesha kuwa gharama za ujenzi ungekuwa Dola za Kimarekani, 47,075,000, kwa mara nyingine utakelezaji wa mradi huo ulikwama kutoka na ukosefu wa fedha.

 Alisema kuwa ndipo, mwaka 2002, NSSF, lilianzisha mazungumzo na Serikali likiwa na nia ya kushiriki katika ujenzi wa daraja hilo. Serikali ililidhia na kulishauri shirika kuanza upembuzi yakinifu kuona kama linaweza kuwekeza katika ujenzi huo.

Alisema kuwa baada miaka kadhaa kufanya pembuzi yakinifu bila mafanikio, ndipo mwaka 2011, Serikali kupitia kwa Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli likubali  kutoa 40% ya ruzuku ya gharama na NSSF kukubali kutoa  60%.

Dk. Dau, alisema kuwa baada ya Serikali kukubali kutoa ruzuku, walitoa tangazo la zabuni ya kutafuta kampuni za kuingia nazo mkataba wa ujenzi wa daraja hilo, ambapo zilijitokza 15, zilizochujwa na kupatikana 7 ambazo pia zilichujwa na hatimaye kampuni ya ujenzi ya China Railway Construction Eng. Group Co Limited kushinda tenda hiyo kwa gharama ya sh. Bil. 214.

Alitaja baadhi ya changamoto zinazoukabili mradi huo kuwa ni;upatikanaji wa wa mapitio ya muda ya barabara wakati wa ujenzi,upatikanaji wa wa eneo kwa ajili ya barabara za maungio upande wa Kurasini na Kigamboni, sehemu ya kutupia udongo  wa ziada wakati wa ujenzi wa daraja na barabara.

Changamoto zingine ni; uhamishaji wa miundombinu mbalimbali katika barabara ya  Nelson Mandela na uboreshaji wa makutano ya  barabara eneo la Chang'ombe, Kamata na Tazara.

Dk. Dau alitoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Nne inayooongozwa na Rais Jakaya Kikwete kwa kukubali kutoa 40% ya ruzuku ya gharama ya ujenzi wa daraja hilo. Pia alimshukuru Dk. Magufuli kwa uamuzi wake na kusimamia vyema hatua za utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Magufuli, aliitaka kampuni ya ujenzi wa daraja hilo, kuhakikisha inakamilisha haraka ujenzi wa daraja hilo kabla ya miezi 36 waliyopewa, ili Rais Jakaya Kikwete alifungue kabla ya kumaliza muda wake 2015.

"Sioni sababu daraja hilo lijengwe  kwa miezi 36, inatakiwa  mlikamishe kabla ya muda huo, kwani iatakuwa ni sifa kwenu, lakini vile vile  nataka Rais Jakaya Kikwete alizindue daraja hilo kabla ya kumaliza muda wake," alisema Dk. Magufuli.

Pia alimsifia Dk Dau kwa ujasiri aliufanya wa kukubali NSSF, kutoa fedha za ujenzi wa daraja hilo, litakalokuwa la kihistoria. Alisema si vizuri kusubiri kumsifia mtu akifa, bali sifa hizo apewe akiwa hai.

Aliwaasa watanzania kuacha kuhubiri siasa na kuwataka wachape kazi, ambapo alinukuu neno la Mungu kwenye Biblia kuwa asiyefanya kazi na asile.

"Mpeni Rais Jakaya Kikwete achape kazi, Siasa zitatuchelewesha, Siasa zitatupeleka pabaya," alimazia kusema Dk. Magufuli.

Mradi huo utasaidia ajira ya watu 3000, wakiwemo wataalamu 1000 na vibarua 2000.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*