NYETI ZA MWANAMKE ZATOWEKA USINGIZINI - MBEYA
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Tunkumbukege
Mbalaswa (20) mama wa watoto wanne mkazi wa kijiji cha Nsongola kata
ya Bujela wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya amekuwa kwenye wasiwasi baada
ya sehemu zake za siri kutoweka usiku wa Desemba 30 mwaka uliopita.
Akiongea
kwa masikitiko Bi Tunkumbukege amesema alijifungua salama kabisa
mtoto wa kiume October 2011 aitwaye Shaban Elia na hakupatwa na tatizo
lolote hadi Desemba 30, mwaka jana alipokutwa na tatizo la sehemu za
siri zikiwa zimeondolewa hali iliyomsababishia maumivu makali na hivyo
kumlazimu kwenda Zahanati ya Bujela na kuonana na Daktari wa zahanati
hiyo na kumpata dawa mama huyo akidai ni ugonjwa wa Fistula.
Baada ya siku saba za matibabu kumalizika hali ya mwanamke huyo iliendelea kuwa mbaya huku sehemu zake za siri zikionekana zimekeketwa na tundu la mkojo kutobolewa na spoko ya baiskeli hali ambayo haja ndogo ikimtoka bila utaratibu na kupata hadha kubwa.
Bi
Tunkumbukege Mbalaswaalijifungua mtoto wa kwanza mwaka 1997, na mtoto
wa pili mwaka 2003 wote wakiwa ni jinsi ya kike, mtoto wa tatu mwaka
2006 na mtoto wa kiume mwaka 2011 wote wakiwa ni jinsi ya kiume
ambapo wote hajapata matatizo yoyote katika uzazi.
Kwa
upande wake Mumewe Bwana Elia Mwambapa amesema matatizo yote
amemwachia Mungu kwani mkewe amekuwa akipata shida licha ya kumaliza
dawa, mkewa hajapata hafueni yoyote.
Uchunguzi
uliofanywa na Daktari amesema katika utabibu wake hajawahi kukumbana
na mgonjwa mwenye tatizo hilo na kwamba baada ya vipimo vya Fistula
amegundua kuwa mgonjwa wake hana ugonjwa huo(Fistula).
Kufuatia
hali hiyo Bi Tunkumbukege anahusisha tatizo hilo na imani za
kishirikina hali ambayo imepelekea kupatiwa matibabu na mganga wa tiba
za asili(jadi)ambaye hakupenda kumtaja jina.
Mkoa
wa Mbeya ni moja ya mikoa ambayo imekuwa ikihusishwa kutawaliwa na
imani za kishirikina, hali ambayo imepelekea wakazi wake kuendelea
kuishi kwa hofu, kutokana na baadhi ya watu kuendekeza kuishi katika
imani hizo na wengine kuuawa na wananchi wenye hasira kali. HABARI KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG
Comments