POLISI ARUSHA WAFANIKIWA KUUA JAMBAZI AMBAYE ALIUWA POLISI,NA KUMJERUHI MPELELEZI MKUU WA WILAYA YA ARUSHA VIJIJINI

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Thobias Angengenye akionesha moja ya silaha ambazo zilikuwa zikitumika na jambazi huyo aliyeuwawa na polisi mapema leo asubuhi.
Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-ARUSHA
JESHI LA POLISI mkoani Arusha limefanikiwa kumuua jambazi sugu ambaye wiki iliyopita naye aliua askari na kumjerui afisa wa jeshi hilo kwa wilaya ya arusha vijijini.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Thobias Angengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea katika eneo la Lalashi kitongoji cha Lengine wilayani Arumeru.
Kamanda Andengenye alieleza kuwa katika tukio hilo jambazi huyo ambaye alifahamika kwa jina la Pokea Samson Kaaya alikuwa alipata majeraha katika sehemu ya mguu ambapo katika siku yatukio alikuwa akijibishana risasi na askari polisi na hivyo akaogopa kwenda hospitalini kwa kuwa angeweza kushikwa kwa uraisi sana.
Andengenye alibainisha kuwa kutokana na hofu hiyo ilimfanya jambazi huyo kutafuta mganga wa kienyeji ambapo alifanikiwa kuingia katika nyumba ya Bi Anna Loshilari katika eneo la Orarashi.
Alisema kuwa kuwepo kwa jambazi huyo katika eneo hilo kulifanya raia wema waweze kutoa taarifa kwa jeshi hilo ambapo polisi walifuatlia nyendo pamoja na taarifa hizo kwa umakini na kuweza kumpata jambazi huyo katika eneo hilo akiwa amelala ndani hali ambayo ilifanya askari kuzunguka nyumba hiyo hadi majira ya saa 6.45 asubui na ndipo jambazi huyo alipotoka huku akiwa anakimbia
Kamanda alibainisha kuwa jambazi huyo alikimbia umbali mrefu sana lakini gafla akanza mapambano na askari kwa nia ya kuchukua silaha na kisha kuwajerui lakini hakufanikiwa kuchukua silaha na badala yake alifanikiwa kumjerui askari wa jeshi hilo kwa kumngata kidole gumba na lkumtoboa jicho hali ambayo iliza mapambano makali sana ambayo yalisababisha kifo chake hapo hapo.
Pia alisema kuwa mara baada ya kufariki askari walifanikiwa kuwakamata watu wanne akiwemo mke wa wa jambazi huyo pamoja na silaha ambazo nazo zilipatikana katika eneo la Moshono ambapo silaha hizo ni pamoja na SMG No 1016188011 , risasi kumi na moja,Shortgun Moja yenye Model 88-12GA,risasi nne ambapo zilikuwa zimehifadhiwa katika mfuko mkubwa wa Salphate huku zikiwa zimefichwa katika eneo la vichaka ndani ya eneo hilo la Moshono.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.