SERENGETI LAGER YAZINDUA NEMBO YENYE MUONEKANO MPYA WA DHAHABU, LAKINI BURUDANI ILEILE

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko B. Joyce Mapunjo katikati akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Kampuni ya bia ya Serengeti mara baada ya kuzindua rasmi bia ya Serengeti katika muonekano wa Dhahabu, uzinduzi uliofanyika jana jioni kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam na kuhudguriwa na wadau mbalimbali na wageni waalikwa.
Kutoka kulia ni Emilian Rwejuna meneja masoko (SBL) Mark Tyro Mkurugenzi wa Usambazaji, Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko, Mgeni rasmi Katibu Mkuu Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo, Mkurugenzi mtendaji wa (SBL) Richard Wells na kushoto ni Zohra Moore Meneja wa Huduma IPP wakipozi kwa picha huku wakiwa wameshikilia chupa mpya ya Serengeti Lager iliyo katika muonekano wa Dhahabu
Chupa mpya ya Serengeti Lager yenye muonekano wa wa Dhahabu ikiibuka kutoka katika maji mara baada ya kuzinduliwa rasmi jana usiku.
Shamrashamra zikiendelea wakati nembo mpya ya bia ya Serengeti Lager ikizinduliwa jana.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko B. Joyce Mapunjo akizungumza katika uzinduzi huo
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells akizungumza katika uzinduzi huo wakati alipomkaribisha mgeni rasmi.
Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti akizungumzia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika taifa kupitia bia ya Serengeti Lager.
Mark Tyror Mkurugenzi wa Usambazaji kulia na Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti wakionyesha nembo mpya ya bia ya Serengeti Lager. Mrembo wa Serengeti Lager akipozi kwa picha na huku akionyesha Nembo mpya ya bia ya Serengeti Lager
Mkurugenzi wa Usambazaji Mark Tyro kushoto akipozi kwa picha na marafiki zake Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells, Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti na Mwisho ni Meneja wa Mahusiano kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela
Hapa ilibaki burudani tu.
Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti akiongea na mkurugenzi wa Extra Bongo Kamalade Ali Choki , kulia ni Meneja Masoko wa (SBL) Emilian Rwejuna.
Hapa mzuka ukapanda kidogo lakini yote ilikuwa burudani na uzinduzi wa muonekano wa Dhahabu katika burudani ileile ya Serengeti Lager.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Kikundi cha ngoma za asili kikitoa burudani katika uzinduzi huo.
Dada Ritah Mchaki meneja wa bia ya Tusker katikati akipozi na wadau kutoka kampuni ya bia ya Serengeti . Chanzo Blog ya Fullshangwe.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA