Sheria ya hali hatari yaondolewa Misri


Hussein Tantawi aondoa sheria ya hali ya hatari

Kiongozi wa jeshi nchini misri amesema kuwa sheria ya hali ya hatari ya miongo kadhaa imeondolewa kwanzia jumatano tarehe 25 Januari wakati wa kuadhimisha harakati zi maandamano zilizomng'oa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo,Hosni Mubarak.

Field Marshal ,Hussen Tantawi, bila kutoa maelezo zaidi, amesema kuwa sheria hiyo itaendelea kutumika kupambana na ujambazi.

Baraza hilo la kijeshi limetumia neno "ujambazi" kuthibitisha tendo la kuwachukulia hatua kali wanaotaka kurejeshwa kwa sheria za raia.

Misri imekuwa chini ya sheria hiyo ya hali ya hatari tangu mwaka wa 1967

Sheria hii iliwapa polisi uwezo wa kupita kiasi wa kupuuza kwa muda haki muhimu kama vile kupiga marufuku maandamano,kuchunguza na kudhibiti vyombo vya habari, kuchunguza mazungumzo ya kibinafsi na kuwazulia watu kwa muda bila mashtaka.

Mubarak alivunja ahadi za mara kwa mara za kuiondoa sheria hiyo ya hali hatari ambayo imekuwa humo tango mauaji ya rais Anwar Sadat kufanyika mwaka wa 1981

Tangazo hilo la Tantawi limetokea siku moja tu baada ya bunge kufanya kikao chao cha kwanza tangu Mubarak kujiuzulu na Baraza kuu la kijeshi kuchukua mamlaka.

"Leo , baada ya raia wa misri kutoa msimamo wao na kuwachaguwa wabunge wao katika baraza la wawakilishi ili kuanza shughuli zao za utunzi wa sheria ,nimechukua hatua ya kuondoa sheria ya hali ya hatari nchini kote. Lakini tutaitumia tuu katika kupambana na majambazi. Hatua hii inaanza kutekelezwa kuanzia hii leo tarehe 25 Januari"

Mwaka uliopita, wakuu hao walijumuisha migomo ya kikazi, usumbufu wa magari na kueneza habari za uongo au uzushi katika sheria hiyo ya hali ya hatari.

Waandishi habari wamesema kuwa kuondolewa kwa sheria hiyo kwa kiasi huenda kukawaridhisha waandamanaji wanaounga mkono demokrasia na makundi ya kutetea haki za kibinadamu.

Mwandishi wa BBC, Jon Leyne akiwa Cairo amesema kuwa neno jambazi linaweza kuwa na maana pana zaidi hivyo haona kama tangazo hilo huenda lisifurahiwe na wapinzani .

Huku kukiwa na bunge jipya baada ya kupiga kura,jeshi nchini humo linaweza kumakinika kwa sasa ukilinganisha na hali ilivyokuwa miezi michache iliyopita, lakini huenda wakatatizwa wanapoadhimisha harakati zilizobadilisha uongozi na siasa za Misri.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA