Sudan: Marais wakutana Addis Ababa

Marais wa Sudan Kusini na Sudan wanakutana mjini Addis Ababa, Ethiopia katika juhudi za kutafuta suluhu kwa tofauti zilizoibuka kati ya majirani hao wawili kuhusu mafuta.

Tangu kujitenga kwake kutoka kwa Sudan, Sudan Kusini imekuwa ikisafirisha mafuta yake kwa mauzo ya nje ya nchi kupitia mabomba ya Sudan.

Hata hivyo makubaliano ya kiwango cha malipo ya gharama ya uchukuzi hayakuafikiwa.

Sudan imelazimika kuchukua bila ruhusa mafuta hayo au kama inavyodai Sudan Kusini kuyaiba.

Kujibu vitendo hivyo Sudan Kusini ilitangaza kusitisha uzalishaji wa mafuta na kutengeneza bomba jipya la kusafirisha mafuta yake kupitia bandari ya Lamu nchini Kenya hatua ambayo huenda ikaathiri uchumi wa mataifa hayo mawili.

Ni kwa maana hii viongozi wa mataifa hayo mawili wanakutana.

Marais wa Kenya na Ethiopia wanaohudhuria mkutano huu watajaribu kuwapatanisha mahasimu hawa wa jadi. Inahofiwa kama hilo halitafanyika kutazuka mzozo mkubwa kati ya majirani hawa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA