SUDANI KUSINI KUPITISHIA MAFUTA KENYA

Sudan Kusini imesaini makubaliano na Kenya kupitisha bomba lake la mafuta ili kupunguza utegemezi kwa jirani yake wa kaskazini Sudan

Litaunganisha visima vyake vya mafuta kupitia bandari ya Lamu nchini Kenya na inatarajiwa kuwa tayari ndani ya mwaka mmoja, waziri wa Sudan Kusini alisema.

Wiki iliyopita Sudan Kusini Sudan Kusini ilisema inasitisha uzalishaji wa mafuta yake kwa sababu ya mgogoro juu ya malipo ya usafirishaji huo.

Tangu Sudan Kusini ijitenge kutoka Sudan mwezi Julai mwaka jana uhusiano wao umekuwa ukiporomoka.

Mwandishi wa BBC James Copnall akiwa mji mkuu wa Sudan Khartoum anasema kutangazwa kwa ujenzi wa bomba jipya kupitia Kenya kutoa ujumbe kuwa Sudan Kusini inaweza kusafirisha mafuta yake bila kutegema Sudan na miundo mbinu yake ya mafuta.

Ugomvi wa gharama za usafirishaji

Hakuna tarehe iliyotolewa ya kuanza kwa mradi huo lakini Elizabeth James Bol, naibu waziri wa Mafuta na Madini wa Sudan Sudan anasema utakuwa ‘mapema iwezekanavyo’.

Aliambia BBC anatarajia kuwa bomba hilo litakamilika kwa miezi 11.

"Bomba hilo litapitia Kenya na litajengwa na kumilikiwa na Sudan Kusini," ilisema taarifa kutoka kwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, ambaye alikuwa Juba kwa ajili ya kusaini makubaliano hayo mchana wa Jumanne.

Sudan Kusini na Sudan – ambazo zilipigana vikali kwa miongo mingi zimeendelea kuwa mahasimu hasa juu ya mafuta ambapo nchi zote mbili zinategemea kwa asilimia kubwa ya mapato yake.

Sudan Kusini ina hazina ya mafuta, na 98% ya bajeti ya inategemea mafuta hayo.

Lakini Kaskazini ina bomba la mafuta, kiwanda cha kusafisha mafuta hayo na bandari ya kusafirishia mafuta ya Port Sudan katika bahari ya Shamu.

Hawajawahi kukubaliana kuhusu kiasi cha malipo ya kusafirisha mafuta hayo ambacho Juba inatakiwa kuilipa Khartoum kwa kupitisha mafuta na matumizi ya miundo mbinu ya kusafirisha mafuta hayo.

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ameishutumu serikali ya Sudan kwa kuchukua mafuta hayo kinyume na sheria, na kudai kiasi cha $815m cha mafuta yake ambayo hayajasafishwa.

Khartoum imekiri kuondoa baadhi ya fedha ambazo hazijalipwa, na Ijumaa iliyopita Sudan Kusini ilitangaza kufunga uzalishaji wa mafuta yake kupitia Sudan.

Rais Kiir alisema afadhali Taifa lake lipate taabu kwa muda kuliko kuendelea kutoa mapato yake kwa adui wa zamani mjini Khartoum.

Waandishi wanasema kuna wasiwasi kuhusu athari za bomba hilo kupitia Lamu ikiwa ni eneo zuri ambalo halijaharibiwa mazingira yake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA