UDHAMINI MNONO WARUDISHA MICHUANO CUP DAR

UDHAMINI mnono unaopatikana Tanzania umelifanya Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kuamua kurudisha Kombe la Kagame jijini Dar es Salaam tena mwaka huu.

Michuano hiyo ya Kagame iliyofanyika mwaka jana na kushuhudia Yanga ikitwaa ubingwa baada ya kuifunga Simba katika fainali huku umeme ukikatika Uwanja wa Taifa, mwaka huu yalipangwa kufanyika Rwanda. 
Akizungumza na gazeti la The New Times la Rwanda, Katibu mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, alisema wameamua kurudisha mashindano hayo Tanzania kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana mwaka jana.

Pamoja na mafanikio ya mashindano hayo, Cecafa pia kuna jambo moja la muhimu la kupatikana kwa wadhamini Tanzania ambao wameshapata siku moja iliyopita.

Taarifa hiyo inalifanya jiji la Dar es Salaam kuwa mwenyeji kwa mara ya pili mfululizo kwa Kombe la Kagame kama ilivyokuwa kwa Kombe la Chalenji lililofanyika mwaka jana na kushudia Uganda 'Cranes' wakitwaa ubingwa huo kwa kuichapa Rwanda.

Zanzibar na Sudan pia walikuwa wakipewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa kwa klabu Afrika Mashariki na Kati, lakini tatizo la fedha limewakosesha nafasi hiyo.

Fainali ya mwaka jana ya Kombe la Kagame, ilizikutanisha timu zote za Tanzania, Simba na Yanga na kushuhudia kocha Sam Timbe akipata taji lake la nne la Kombe la Kagame baada ya kufanya hivyo akiwa na SC Villa (2005), Polisi (2006), Atraco (2009) na Yanga (2011).

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Kenneth Asamoah alikuwa shujaa baada ya kuingia akitokea benchi na kufunga bao la kichwa kwenye muda wa nyongeza.

Tangu mwaka 2002, rais wa Rwanda, Paul Kagame amekuwa akifadhiri mashindano hayo kwa kutoa dola 60,000 kama zawadi kwa washindi.

Mapema wiki hii Cecafa pia ilithibitisha Kombe la Chalenji mwaka huu litafanyika katika mji wa Kisumu, Kenya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA