Ummy: Moto wa Twiga Stars hadi ubingwa wa Afrika

MRATIBU na Mhamasishaji wa timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, Ummy Mwalimu amesema mto uliowashwa na timu hiyo kuitoa Namibia kwa kishindo cha mabao 7-2 utazimwa watakapokuja na Kombe la Afrika Tanzania.

Akizungumza na Mwananchi kwenye Uwanja wa Taifa juzi jioni, Mwalimu ambaye ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto alisema kuwa Twiga Stars wamefanya kazi kubwa na kuweka heshima Tanzania na Afrika na kuonyesha wanawake wanaweza.

Twiga Stars iliitoa Namibia kwa jumla ya mabao 7-2 katika mchezo wa marudiano uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo Mwalimu ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tanga alisema: "Sijui niseme nini...nimechanganyikiwa au niseme nimepagawa kwa ushindi, lakini bado nasema hatujamaliza, kazi ndiyo imeanza.

"Moto mliowasha nataka muuzime kwa kombe litakapokuja nchini...vyote vinawezekana.
Mmeonyesha mnaweza na nawashukuru Wabunge Marafiki wa Twiga Stars, nimeunganisha Wabunge 40 kutengeneza mtandao na kweli unafanya kazi. Wanawake tukiwezeshwa tunaweza," alisema Mwalimu.

Alimshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Emmanuel Nchimbi kwa kumruhusu kuingia kwenye timu hiyo huku akirejea kuwashukuru wabunge wengine kwa kazi hiyo.

Alisema kuwa pamoja na kuwapatia wachezaji Sh1mil ikiwa ni ahadi ya kama wangekuwa wa kwanza kufunga, bado ataendelea na kampeni ya kuhamasisha kuisaidia timu hiyo kwa kutia hamasa wabunge 40 waliopo katika mtandao na wengine zaidi kuichangia timu hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA