Utafiti uliofanywa na wataalamu wa Marekani umebaini kuwa wanawake wanaoishi kwa matumaini hupunguza uwezekano wa maradhi ya moyo.

Utafiti wa hivi karibuni wa watafiti wa Marekani unakariri utafiti wa awali uliofanywa na kundi la wataalamu wa Uholanzi ukionyesha kupungua kwa uwezekano wa hatari ya magonjwa ya moyo kwa wanaume.

Utafiti uliofanywa kwa kutumia wanawake laki moja,ulichapishwa katika jarida la kisayansi, uligundua kuwa watu wanaoishi kwa hofu walipatikana kua na shinikizo la damu pamoja na kolestroli au kupungua kwa njia za damu katika mishipa.

Pamoja na hayo hisia za mtu kama tabia ya chuki kwa wengine pia yanabadili hali ya afya.

Wanawake wenye matarajio mema wana asili mia 9% ya kupatwa na magonjwa ya moyo na asili mia 14% ya kuuawa kwa magonjwa yenye uhusiano wa maradhi ya moyo.

Wanawake wa aina hiyo walilinganishwa na wengine ambao huishi kwa kinyongo, chuki na kijicho kwa wenzao kimawazo au kwa ujumla kuwashuku wenzao. Hawa wana asili mia 16% kufariki katika kipindi kifupi kuliko wanaoishi kwa matumaini makubwa ya kufanikiwa.

Uwezekano mkubwa uliopo ni kwamba mtu anayeishi kwa matumaini huwa na uwezo wa kukabiliana na mitihani ya kimaisha, mfano wa kukidhi mahitaji yao wanapoumwa.

Utafiti huu ulionelea kuwa wanawake wanaofanya mazowezi mara nyingi walikuwa wembamba kuliko wenzao wanaoishi na kinyongo.

Mchunguzi mkuu Dr Hilary Tindle, naibu profesa wa dawa katika Chuo kikuu cha Pittsburgh, alisema kua ushahidi mwingi tulioupata unaonyesha kua muendelezo kwa kiwango kikubwa cha fikra za kutojiamini ni hatari kwa afya."

Msemaji wa shirika la Uingereza ''British Heart Foundation alisema kua: "tunafahamu kuwa chuki na unyonge husababisha kemikali fulani mwilini ambazo zinaweza kuzidisha uwezekano wa maradhi ya moyo, ingawa hatuelewi kikamilifu ni kwanini.

Matumaini au hata chuki ni hisia zinazoweza kuambatanishwa na tabia zinazokubaliana na afya njema, uvutaji sigara au chakula kibovu ambavyo vyote vinaweza kuchangia katika afya ya moyo.

"habari njema kwa wanawake ni kua mbali na sura yako, chaguo lako katika maisha mfano wa chakula au kutovuta sigara kuna athari kwa moyo usiokua na matatizo kuliko kua na uso mrembo.

Bado kuna hitajika uchunguzi zaidi kujifunza sababu hisia za aina hii huathiri afya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA