Vita vyaingia vitongoje vya Damascus

Taarifa kutoka Syria zinaeleza kuwa jeshi la serikali likiwa na vifaru linashambulia sehemu za upinzani mashariki na kaskazini ya mji mkuu, Damascus.

Mpinzani wa serikali nchini Syria

Wanaharakati wanasema watu kama 13 wameuwawa leo.

Wanaharakti wanasema wanajeshi zaidi ya 2000 na vifaru 50 vilishiriki katika shambulio hilo liloanza alfajiri, kwenye vitongoje kama kilomita tano mashariki ya Damascus.

Wanasema vifaru na mizinga ilishambulia maeneo hayo, ambayo yalizingirwa na kutengwa, na umeme na mawasiliano yalikatika.

Baadhi ya vitongoje hivo vimekuwa ngome za harakati za wapiganaji wa Jeshi Huru la Syria, ambalo linajumuisha wanajeshi walioasi kutoka jeshi la serikali.

Kuna taarifa kama hizo kutoka mji wa Rankous, ulioko milimani, kilomita 30 kaskazini ya Damascus.

Wanaharakati wanasema mji wa Rankous umekuwa eneo la vita, na wanaomba msaada na madawa ya kupeleka huko.

Mapambano hayo yanatokea bila ya mashahidi kutoka nchi za nje kwa vile ujumbe wa wachunguzi wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu umeambiwa na makao makuu ya jumuia kuwa usimamishe shughuli zake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA