Mazishi ya Mbunge wa Chadema, Mheshimiwa Regia Mtema
yamethibitisha kuwa vituko na vioja vya Katibu Mkuu wa Chadema,
Mheshimiwa Wilbroad Slaa na “mchumba wake,” Josephine Mushumbusi
havijaisha hata kama sasa wanaishi pamoja.
Kwa namna ambayo sasa imethibisha nani hasa mwenye madaraka, mamlaka
na kauli ndani ya nyumba yao, Josephine Mushumbusi amemzuia
“mchumba/mume” kwenda kumpa mkono Kiongozi wa nchi, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Mara baada ya Rais Kikwete kuingia
katika makaburi ya familia ya Mtema mjini Ifakara kiasi cha saa tisa
unusu mchana, Mheshimiwa Slaa ambaye alikuwa amekaa peke yake na
Josephine pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema,
alionyesha ishara ya kwenda kumsalimia Mheshimiwa Rais Kikwete ambaye
alikuwa jukwaa kuu.
Lakini Josephine Mushumbusi alimzuia mchumba wake asiende kumsalimia Rais Kikwete akimwambia, “usiende…italeta maneno ya bure.”
Kwa namna inayothibitisha nani bosi ndani ya nyumba, Mheshimiwa Slaa alijikunja na kusalimu amri akisema, “haya bwana”.
Kila dalili za tukio hilo zimethibisha
kuwa ubabe na ushujaa ambao Mheshimiwa Slaa huonyesha hadharani kwa
kutukana, kukejeli na kuwashambulia wenzake katika siasa akiwamo Rais
Kikwete ni nguvu za soda tu zisizotamba mbele ya Josephine ambaye
alionyesha udhitibi na umwamba wake hadharani leo.
Lakini tukio la leo pia limethibitisha
kwa mara nyingine kiwango cha kinyogo ambacho familia ya Slaa na mchumba
wake wanayo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kikwete
tokea Rais alipowabwaga na kumsambaratisha kwa kishindo katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka juzi, 2010.
Tokea wakati huo, Mheshimiwa Slaa
hajapata kumsema vizuri Rais Kikwete, hajapata hata kumtambua hadharani
pamoja na kujua kuwa alishindwa kihalali, hajapata kumsalimia wala kumpa
Kiongozi huyo wa nchi mkono hadharani hata fursa inapojitokeza kama
leo.
Kwa ufupi, tukio la leo na mengine mengi yalimtangulia limethibitisha
kuwa Mheshimiwa Slaa ni kiongozi mwenye kinyongo na asiyekuwa na heshima
kabisa.
Kama ambavyo wamepata kusema wengine hana sifa za kuwa na kiongozi mkuu
wa nchi yetu hii inayoongozwa kwa misingi ya maelewano na siyo kwa
misingi ya chuki ambazo anazionyesha Mheshimiwa Slaa. Kwa hili Dr. Slaa
Kachemsha, kadhihirisha wazi kuwa hana siyo tu ukomavu wa uongozi bali
pia ukomavu wa kisiasa. Sasa naelewa pia kwa nini Slaa upadre
ulimshinda.
Ni jambo la ajabu kuwa mfiwa kama
alivyokuwa Slaa leo kwa sababu yeye amempoteza Mbunge anakataa vipi
kwenda kumsalimia mwombolezaji ambaye amekwenda kumpa pole na kumjulia
hali. Huu ni ubinadamu na uungwana kweli?
Mzee Slaa anashindwa na wadogo zake
kama vile Mheshimiwa Freeman Mbowe na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe
ambao walipeana mikono na kukaa pamoja na Mheshimiwa Rais, kubadilishana
mawazo na kuomboleza kwa pamoja.
|
Comments